Rubani msaidizi wa ndege
ya Ethiopian Airlines iliyokuwa ikienda Roma toka Addis
Ababa ameteka ndege hiyo mapema leo na kuilazimisha itue Geneva , Uswisi, polisi
wameieleza AFP.
Rubabi huyo alitenda
kitendo hicho cha ajabu kama njia ya kujaribu
kuomba hifadhi ya kisiasa nchini Uswisi. “Anadai anaishi kwa hofu nchini kwake
mwenyewe, hivyo anataka hifadhi Uswisi,” vyanzo vya kipolisi vimeiambia AFP.
Tukio lilivyotokea
Wanausalama Geneva
wanasema rubani huyo msaidizi alivizia mwenzake alipokuwa amekwenda kujisaidia,
kisha akajifungia katika chumba maalum cha kuongoza ndege na kubadili uelekeo
wa chombo hicho kukipeleka Uswisi.
Baada ya hapo, kijana
huyo mwenye umri wa miaka 31 ambaye ni raia wa Ethiopia
aliomba idhini ya kutua Geneva
akidai anahitaji mafuta ya dharura. “Ghafla, akatutangazia kuwa ameteka ndege,”
vimesema vyanzo hivyo.
Safari zasimama, huduma
zavurugika
Kutokana na hati hati
hiyo, ilibidi safari zote kuingia na kutoka uwanjani hapo zisitishwe mapema
leo. Hata hivyo, kufikia saa 2:45 asubuhi kwa saa za ulaya ya kati, hali ya
utulivu ilishaanza kurejea.
Polisi wamemtia ndani mteka ndege huyo, ambaye
anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu ijayo, zasema taarifa zilizoifikia

No comments:
Post a Comment