KALI ZA USWAZI

PAYMENT FOR SIN
[MALIPO YA DHAMBI]

MTUNZI: Fortunatha Sixberth
MWANDISHI: ngoogle Shakur +255712 554 944
Email: ngogoshakur@yahoo.com

SEHEMU YA KWANZA 01
K
elele za nguvu zilisikika kutoka katika chumba  Kadri zilivyozidi kuendelea ndivyo umati wa watu ulivyozidi kufurika kuelekea eneo lile. Ama kwa hakika ilikuwa ni kama sinema ya aina yake kwa mchana ule.
‘Amezoea huyu, leo wacha nimuoneshe kuwa mimi ni zaidi yake’ sauti ya mwanamke ilisikika toka mule ndani. Sauti ile ilizidi kuhamasisha waliokuwa nje ya chumba kile kutaka kujua kulikoni? Lakini muda ulizidi kuyoyoma na hakuna aliyepewa fursa ya kuingia ili angalau aje kuwa shahidi wa kuusimulia umma uliokuwa pale juu ya kilichokuwa kikijiri mule ndani. “Niachie basi mke wangu…” sauti nzito ya kiume ililalamika toka ndani ya chumba kile ikishadidia mawazo ya waliokuwa nje kuwa ndani ya chumba kile mlikuwa na mpambano mkali kati ya mwandamu wa kike na wa kiume.
Wakati hayo yakijiri, wadau baadhi toka kundi la waliokuwa nje walitoa wazo kuwa ni vema kwenda kumtarifu mjumbe wa nyumba kumi ili aje kutoa amri ya kuvunja mlango ili kumaliza mtafaruku ule kwa lazima bila ridhaa ya wahusika. Ndio ni kwa lazima bila ridhaa ya wahusika kwakuwa wenyewe walifunga mlango na komeo zote na hawakuwa tayari kuonesha wengine kilichokuwa kinajiri ndani mule.

Ghafla sauti ya juu ilisikika‘maaaama weeee unaniuaaaaaa!
Hii ilikuwa ni sauti ya mwanamke ikiashiria kuwa alichofanyiwa kilikuwa kinauzito sawa na kumpotezea uhai wake.
Jamani tufanye maamuzi magumu tuvunje mlango watakuja kuuwana hawa….sauti ya msamaria mwema mmoja ilijaribu kuchangia wazo. Hapana wewe utakuja kutukanwa buuuure we unajua ugomvi wa wapendanao? Huwezi jua unavunja mlango kumbe watu wamo katika raha zao…..huyu allikuwa na wazo la tofauti kabisa. Mwingine naye aliibuka na lake ‘Msilete utani bhana, mi navunja mlango na kama kitatokea chochote liwalo na liwe” alimalizia. Kweli bwana fanya hivyo….sauti za akina mama pamoja na wadada zilisikika kuashiria kukubaliana na wazo la kaka yule aliyeonekana kuwa na mwili wa kishababi ambao kama angeamua basi ni wazi angeweza kufanya bila shaka kile ambacho amekitolea tamko dakika chache zilizopita.
Akiwa anajiandaa kufanya kile ghafla sauti zilitamka…Afadhali umefika, maana kila mtu alikuwa na wazo lake hapa. Bila kujibizana na mtu mtu yule alijisogeza kunako mlango na kugonga kwa nguvu….ngongongo! Kimyaa alirudia tena na tena lakini waapi hakuna aliyejibu. Naomba Kijana mwenye nguvu avunje mlango huu haraka…alisema mjumbe  na bila kupoteza wakati Kijana mmoja mwenye umbo lililojaza alijisogeza karibu na mlango ule na aligeuka kutazama umma uliojaa pale kasha kimzaha aliruka kinyume nyume na kwa kutumia makalio yake akauvamia mlango. Puuu! Sauti hiyo ilisikika na bila chenga watu waliweza kuona japo kwa uchache mandhari ya ndani ya chumba kile ambacho kilikuwa kikisikika sauti zenye kuashiria patashika nguo kuchanika muda si mrefu uliopita. Naomba vijana watatu wenye nguvu ongozana nami pamoja tukashuhudie kulikoni….mjumbe aliita kundi la vijana na hakukupita sekunde tayari waliongozana kuingia ndani.
Mamaaa weee! Huyu si mzima tena. Ameshakata pumzi huyu au sio bwana mjumbe? Kijana mmoja alidadisi. “Bila shaka itakuwa hivyo lakini tusimalize kila kitu kwa uwa ssi sio madaktari tuwaachie kazi hiyo wahusika watatupa jibu sahihi kabisa”
Mjumbe hakutaka kupoteza muda ndani ya dakika tatu alipiga simu kituo cha polisi na difenda ilikuwa tayari eneo la tukio kuchukua wahusika. Ndani ya diffenda kulikuwa na afande Katosho ambaye alikuwa  pamoja na afanse wa kike Zipora. Kundi la mashuhuda lililokuwa hapo awali limezunguka nyumba ile baada tu ya kufika gari la polisi lilionekana kusambaratika na kuacha eneo lile kubaki na watu wachache huku umati ukiwa kwa mbali mbali.
Makamanda hawa hawakutumia muda mwingi walishaingia ndani ya chumba cha tukio na punde vijana waionekana wakibeba miili mitatu kuingiza katika gari. Miili ile ilionekana wazi kuwa ni wanawake wawili na mwanamume mmoja. Gari la polisi liliondoka kwa mwendo wa kasi ili kujaribbu kuokoa maisha ya wahanga wa tukio lile.

Umati uliobaki eneo lile uliachwa na maswali mengi yasiyo na majibu…ni akina nani basi waliokuwa katika tukio lile? Hali za watu wale zilikuwaje yaani ni wazima au wote wamefariki? Na wengine walikwenda mbali zaidi na kujiuliza kisa namkasa cha tukio lile. Lakini maswali haya hayakupata majibu kutokana na ukweli kuwa wahusika ndio wale walikuwa hawajitambui wakati wakitolewa eneo lile na hata wale vijana watatu waliosaidia pengine ndio angalau wangeeleza lolote nao walichukuliwa na ili kwenda kusaidia taarifa muhimu kituoni.
Basi hakukuwa na jinsi ilibidi kila mmoja achukue njia yake huku wabunifu wakijaribu kueleza uongo usiosanifu juu ya tukio lile……………USIKOSE SEHEMU YA 2

No comments:

Post a Comment