Dec 11, 2013

VIGOGO WAFURAHIA LAANA YA KANGA MOKO NDEMBENDEMBEEEEE???



Mswahili mwenzangu, kama kuna watu ambao wanajitahidi kwa kiasi  kikubwa kuharibu maadili ya Mswahili ni hawa dada zetu wanaojiita KANGA MOJA LAKI SI PESA. Kwa mujibu wa wanaohudhuria maonesho ya wadada hawa ni kwamba zaidi ya laana watendayo basi hakuna lingine.

Siku za hivi karibuni kundi hilo limezidi kujipatia umaaufu kiasi hata katika simu za watu kuwemo picha ama video zinazowaonesha wadada hao wakijiachia Kihasarahasara katika kumbi zenye umma wa watu.

Swali langu; kama weli kuwa hayo machafu ndiyo yafanywayo na hao Wakali wa laki SI pesa, basi NI NANI KATIKA UTAWALA (serikali) mwenye mamlaka ya kuzuia matendo machafu kama haya????

Ni wazi kuwa kuyaacha yaendelee ni sawa na kutangaza kuwa jamii yetu sasa imekuwa sawa na jamii ya wale nyani au sokwe walio mwituni ambao kiasili hawakujaaliwa kujistiri na kuwa na tamaduni za kistaarabu kama zetu Waswahili. INASIKITISHA SANA….akina dada hao kuonekana wakijiachia kiasi cha kuwa ni sawa na kufanya ngono hadharani na cha kushangaza picha zao pamoja na video za uchafu wao zimekuwa zikishamiri mitaani kila kukicha na WAHUSIKA KUTOCHUKULIWA HATUA YOYOTE.

HIVI SERIKARI INAFANYA NINI AU NDIO VIGOGO WANAONA UTAMU KWA HAYA MACHAFU WATENDAYO HAWA WACHAFUZI????

Wahusika mnapaswa kutambua kuwa mlipewa mamlaka yenye kuwapa nguvu za kisheria za kusimamia UADILIFU katika jamii hii. Kukaa kwenu kimya mtakuja kushangaa waliowapa mamlaka siku moja WANACHUKUA NAFASI ZENU NA KUFANYA KAZI WALIYOWAPA KINGUVU….,AMKENI VIONGOZI MLIOLALA NA KUPUMBAZWA NA SIFA ZA KI**

No comments:

Post a Comment