TAHADHARI: PICHA ZINAHUDHUNISHA SANA
Mswahili mwenzangu, wakati
tunaelekea kuufunga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2014 tunapaswa
kufahamu matukio makubwa ambayo kila mmoja wetu amepata kutenda ili kuweza
kujiandaa vema na mwaka huo.
Wakati waja wema tukijaribu
kutafakari juu ya jema lipi ambalo tumelifanya mwaka huu na lipi litaweza
kuvunja rekodi hiyo kwa mwakani, tunapaswa kukumbuka pia kuna matukio ya
kutisha ambayo yamepaswa kutokea katika Jamii zetu.
Mojawapo ni tukio hili hapa
la watu wasiojulikana kumuua kikatili mtu mmoja kwa kumchinja na
kutokomea kusikojulikana na kichwa cha mtu huyo.Baadhi ya askari polisi wakitelemsha maiti ya mtu ambaye
ameuawa kwa kukatwa kichwa na watu kutoweka na kichwa chake usiku wa
kuamkia leo kwa ajili ya kuhifadhi katika hchumba cha kuhifadhia maiti kwenye
hospitali ya mkoa iliyopo mjini Sumbawanga.
Mwenyekiti
huyo aliongeza kuwa watu hao baada ya kufanya mauaji hayo walikwenda kumtupa
kwenye eneo hilo
ambapo asubuhi ya kuamkia leo ndio kiwiliwili chake kilibainika kuwepo hapo
lakini hakina kichwa kwani waliondoka nacho.
Kwa upande wake, Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema kuwa polisi inaendelea kuwasaka watu waliohusika na tukiohilo hili hatua ziweze kuchukuliwa
Kwa upande wake, Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema kuwa polisi inaendelea kuwasaka watu waliohusika na tukio
INASIKITISHA LAKINI TUACHANE
NA MAMBO HAYA YA KIKATILI TUMRUDIE MOLA WETU MWAKA UJAO ILI TUJENGE HIMAYA BORA
YA WASWAHILI, MATUKIO MABAYA KAMA YABAKI KUWA HISTORIA KWA WENZETU YAMETOKEA
No comments:
Post a Comment