Watu kadhaa wamehofiwa kufariki
kufuatia mlipuko uliotokea ndani ya gari moja dogo la abiria katika mtaa wa
Pangani mjini Nairobi .
Duru zinaarifu kuwa karibu watu 4 huenda
wamefriki katika shambulizi Shirika la msalaba mwekundu limesema kuwa watu 15 waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini.
Hata hivyo polisi hawajatangaza idadi rasmi ya watu waliojeruhiwa wala wale waliofariki.
Mlipuko huo umesemekana kutokea ndani ya matatu iliyokuwa inakwenda katika mtaa wa
Athari za mlipuko huo hazikuyasaza magari mengine manne yaliyokuwa karibu na matatu hiyo.
Polisi walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya watu waliokusanyika katika eneo la shambulizi kujionea yaliyokuwa yanajiri.
No comments:
Post a Comment