Jana, Mwili wa hayati Nelson
Mandela ulipelekwa katika mkoa wa Eastern Cape kwa
safari ya mwisho kabla ya kuzikwa siku ya Leo Jumapili kijijini Qunu.
Idadi kubwa ya watu walifurika barabara
angalau kumtupia jicho shujaa wao na kutoa heshima zao za mwisho.Mandela aliyefariki tarehe tano Disemba atafanyiwa maziko ya kitaifa siku ya Jumapili,
Takriban watu 100,000 walitoa heshima zao za mwisho kwa Mandela mjini
Kijiji cha Qunu
Kijiji cha Qunu ambako anazikwa Hayati Nelson
Mandela, kinaomboleza kifo cha shujaa aliyetoka katika kijiji hicho Nelson
Mandela.Mazingira ni ya kipekee, mchanganyiko wa nyumba za kisasa na za kitamduni ambazo mfano wake ni mizinga ya Nyuki.
Visima vya maji anavyovikumbuka Mandela bila shaka hawezi kuviona sasa. Lakini viwanja vya kijiji hiki viko chini ya majabali ambayo yeye na rafiki zake walikesha wakichezea.
Ni viwanja hivi ambapo Madiba alijifunza kuwinda Ndege , kuchukua asali misituni na matunda ya misitu ambayo ilikuwa inaliwa wakati huo.
Alipokuwa na umri wa miaka 5, Mandela aliandika kumbukumbu zake kuhusu safari yake alivyopigania uhuru wa Afrika Kusini, pia alijifunza kuchunga Ng’ombe, na kupitia kwa kazi hiyo alijifunza uhusiano uliopo kati ya watu wa kabila la AbaTembu na Ng’ombe wao.
Alisomea hapa Qunu, lakini kijiji alichokiacha kwa huzuni wakati alimzika babake kimebadilika. Lakini aliporejea hapa mwaka 1990 alipokuja kutembelea kaburi la mamake , alisema aliona umasikini mkubwa machoni mwa watu wa Qubu, viwanja visafi alivyovikumbuka havikuwepo tena, vilikuwa vimejaa takataka kitu ambacho hakuwahi kukiona tangu alipokuwa mtoto.
Hata hivyo Kijiji cha Qunu bila shaka kimebadilika pakubwa, ni kisafi kikubwa na kina dalili za maendeleo, wala sio taswira aliyoitoa Mandela katika kumbukumbu zake kuhusu nyumbani.
Na sababu moja ya
No comments:
Post a Comment