Mswahili mwenzangu hebu nawe
tazama picha hii ya Diwani aliyeuawa kikatili hapahapa Tanzania yetu ambayo tunajinadi
kuwa ni kitivo cha AMANI. Ni wazi kuwa kwa hatua hii tuliyofikia ya kuweza
kutoana uhai wenyewe kwa wenyewe MIOYO YETU IMEJIVIKA UALSHABAB bila
kujitambua. Nijuavyo mimi, katika Jamii yetu hii ya Waswahili ilikuwa ni ngumu
kushuhudia damu ya mtu ikimwagika kirahisi hivi hasa ya KIONGOZI WETU.
Ama kwa hakika tunahitaji
kuzitafakari Noyo zetu na kurejea kule tulikotoka.
JAHAZI LA MSWAHILI linaungana
na serikali kukemea vitendo vya uchukuaji sheria mkononi kwani hatua za
Kisheria zipo Nchini hivyo kwa kila linalojiri bai Wananchi tuachie dora
ichukue nafasi.
Poleni sana familia ya Marehemu ni mipango yake
Muumba.
Na: Domo la Mswahili.
No comments:
Post a Comment