Dec 22, 2013

MAN UNITED YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI ENGALND



Adnan Januzaj akishangilia baada ya kuifungia Manchester United dhidi ya West Ham
Manchester United imeendeleza wimbi la ushindi katika mechi ya nne mfululizo, baada ya leo kuilaza West Ham mabao 3-1 Uwanja wa Old Trafford.
Danny Welbeck alifunga bao la kwanza nyumbani tangu Oktoba 2012 dakika ya 26 na Adnan Januzaj akafunga la pili dakika ya 36 kabla ya Ashley Young kumaliza kazi kwa bao la dakika ya 72 na Carlton Cole akaifungia West Ham bao la kufutia machozi dakika ya 81.

No comments:

Post a Comment