Timu za Kenya na Sudan zimefuzu kucheza fainali za
Shirikisho la Kandanda kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, CECAFA mwaka 2013.
Katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali
uliochezwa uwanja wa manispaa Mombasa kati ya Sudan na Zambia,
Sudan
ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1. Nayo Kenya,
iliweza kujipatia bao la mapema kabisa katika dakika ya tano ya mchezo, wakati
walipopambana na Kilimanjaro Stars ya Tanzania. Hivyo hadi mwisho wa
mchezo, Harambee Stars ilikuwa imepata ushindi huo wa bao 1-0. Mchezo kati ya Tanzania
na Kenya ambao awali ulikuwa
ufanyike katika uwanja wa Machakos, ulihamishiwa katika uwanja wa Nyayo mjini Nairobi, kutokana na
uwanja wa Machakos kuwa katika hali mbaya baada ya mvua kubwa kunyesha. Timu ya Tanzania
na Zambia
zitakutana katika mchezo wa kumpata mshindi wa tatu. Kuingia nusu Fainali Tanzania iliwatoa mabingwa watetezi the Cranes
ya Uganda huku Zambia ikiwaondoa Burundi. Katika hatua hiyo pia Kenya waliweza kuwacharaza Rwanda, huku Sudan
ikiwavurumisha Ethiopia
nje ya michuano hiyo maarufu kwa kanda ya Afrika Mashariki. Zambia ni timu
waalikwa katika mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment