Dec 12, 2013

MAOMBOLEZO YAENDELEA A/KUSINI KWA SIKU YA PILI

 
Waombolezaji nchini Afrika Kusini wanaingia siku ya pili katika zoezi la kutoa heshima za mwisho kwenye mwili wa Rais wa kwanza mweusi nchini Afrika Kusini Hayati Nelson Mandela.
Maelfu ya watu wamejipanga kwenye mistari wakisubiri kutoa heshima zao za mwisho kwenye mwili huo uliolazwa katika ikulu kwenye jengo la Muungano mjini Pretoria.
Mjane wa Marehemu Graca Machel na Rais wa sasa wa Afrika Kusini Jacob Zuma, viongozi wa serikali na wanafamilia walikuwa ni miongoni mwa waliotoa heshima zao za mwisho kwenye mwili wa Marehemu Mandela siku ya jumatano.Viongozi mbali mbali pamoja na raia wa Afrika Kusini walianza kutoa heshima zao za mwisho kuanzia jumatano
Kabla ya kuwekwa katika jengo la ikulu awali mwili huo ulichukuliwa katika msafara kutoka chumba cha maiti cha hosptali hadi kwenye jengo la Muungano.
Msafara wenye jeneza la Marehemu uliondoka mjini katika Hosptali ya jeshi muda mfupi siku ya jumatano. Jeneza lilibebwa kwenye gari maalum na kufunikwa bendera ya Afrika Kusini.
Wananchi walijipanga kando kando ya barabara lilipopitishwa jeneza kama ishara ya kutoa heshma za mwisho kwa mwili wa marehemu.
Msafara ulipita katika mitaa huku baadhi ya raia wakikimbia pembeni kwenye mstari wa askari wa wanajeshi Mwandishi BBC's Joseph Winter katika mji wa Pretoria amesema.
Wanajeshi waliobeba jeneza hilo walisonga hatua kwa hatua hadi katika Majengo ya Muungano eneo alikoapishwa kuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika kusini 1994.
Marehemu Mandela atazikwa nyumbani kwake katika kijiji Qunu katika jimbo la Cape Mashariki siku ya jumapili.
Watu  nchini  Afrika  ya Kusini  wamekusanyika  kwa  siku ya  pili  leo kutoa  heshima  zao  za  mwisho  kwa  mwili  wa rais  wa  zamani  wa  nchi  hiyo  Nelson Mandela  ambao umewekwa  katika  jengo  la  makao  makuu  ya  serikali mjini  Pretoria.
Polisi  wamewekwa  barabarani  katika  gwaride  la heshima  wakati   jeneza  la  Mandela  likirejeshwa  katika jengo  hilo  la  serikali  katika  msafara  maalum, baada  ya kuhifadhiwa  katika  hospitali  ya  jeshi.  Nje  ya  jengo  hilo la  serikali, watu  walikuwa  wakisubiri  kuuona  mwili  wa Mandela  kuanzia  asubuhi  leo. Wanajeshi  walikuwa  wa  kwanza  leo  kuruhusiwa  kutoa heshima  zao.
Rais Jacob Zuma, mjane  wa  Mandela,  Graca Machel,  na mke  wa  zamani  wa  Mandela, Winnie  Madikizela, walikuwa  wa  kwanza  jana  kuuona  mwili  wa  Mandela, wakifuatiwa  na  viongozi  kadha  wa  mataifa  ya  Afrika pamoja  na watu  wengine  mashuhuri.

No comments:

Post a Comment