MWANAFUNZI wa kidato cha tatu
katika shule ya Bujingwa, iliyopo Nyakato Mwanza (jina linahifadhiwa), mkazi wa
Mabatinijijini Mwanza, alibakwa, kutoroshwa nyumbani kwao na hatimaye kupewa
mimba na mtu aliyefahamika kwa jina la Roja (27).
Akizungumza na gazeti hili
hivi karibuni jijini Mwanza akiwa hoi kimaisha baada ya kufukuzwa kwa mwanaume
huyo, denti huyo ambaye sasa ana mtoto mwenye umri wa miezi saba, alisema baada
ya kutoroshwa kwao, mwanaume huyo alimpa mateso mengi, ikiwa ni pamoja na
vipigo vya mara kwa mara.Akisimulia kwa masikitiko, alidai kuwa Roja alimpa
mimba akiwa bado mwanafunzi wa kidato cha tatu mwaka 2012 na kumshawishi
atoroke nyumbani kwao ili akaishi naye.
Alidai kuwa, usiku wa Desemba 9 mwaka huu, Roja akiwa na baba, alifika nyumbani na kumtaka aondoke mara moja huku akimtupia virago vyake nje ya nyumba bila kujali kuwa na kitoto kichanga.“Siku hiyo alifika nyumbani na kunitaka niondoke , nilipokataa akaanza kunipiga na chuma kichwani na kunikaba shingoni bila kujali nilikuwa na mtoto mgongoni. Nilipoona hali inazidi kuwa mbaya nikaamua kuondoka zangu na kuja hapa ili nisaidiwe,” alisema mwanafunzi huyo ambaye wakati huo alikuwa katika ofisi za taasisi inayojishughulisha na utetezi wa haki za binadamu iitwayo Farijika.
Katika kuchimba ukweli wa madai hayo, Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ilizungumza na wazazi wa denti huyo ambao kwa muda tofauti walikiri taarifa za mtoto wao kutoroshwa na kubakwa hadi kuzalishwa na mwanaume huyo.Kuhusu manyanyaso anayopata mtoto wao, walisema anastahili matibabu (PF3) ambapo vipimo vilionesha kuwa kweli alifanyiwa vitendo hivyo kwa kuwa alikuwa na majeraha ya ndani kwa ndani.
Baada ya kuthibitishahilo , Roja aliitwa mbele
ya watetea haki hao na kukiri kumnyanyasa mkewe lakini akiahidi kutomnyanyasa
tena kabla ya kusaini hati ya makubaliano iliyoshuhudiwa na mashahidi watatu,
hati ambayo kama akiivunja atafikishwa
mahakamani kwa makosa mbalimbali ikiwemo kubaka na shambulio la mwili.
Alidai kuwa, usiku wa Desemba 9 mwaka huu, Roja akiwa na baba, alifika nyumbani na kumtaka aondoke mara moja huku akimtupia virago vyake nje ya nyumba bila kujali kuwa na kitoto kichanga.“Siku hiyo alifika nyumbani na kunitaka niondoke , nilipokataa akaanza kunipiga na chuma kichwani na kunikaba shingoni bila kujali nilikuwa na mtoto mgongoni. Nilipoona hali inazidi kuwa mbaya nikaamua kuondoka zangu na kuja hapa ili nisaidiwe,” alisema mwanafunzi huyo ambaye wakati huo alikuwa katika ofisi za taasisi inayojishughulisha na utetezi wa haki za binadamu iitwayo Farijika.
Katika kuchimba ukweli wa madai hayo, Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ilizungumza na wazazi wa denti huyo ambao kwa muda tofauti walikiri taarifa za mtoto wao kutoroshwa na kubakwa hadi kuzalishwa na mwanaume huyo.Kuhusu manyanyaso anayopata mtoto wao, walisema anastahili matibabu (PF3) ambapo vipimo vilionesha kuwa kweli alifanyiwa vitendo hivyo kwa kuwa alikuwa na majeraha ya ndani kwa ndani.
Baada ya kuthibitisha

No comments:
Post a Comment