Mar 18, 2014

ULIISOMA HII??? SIMU YAUA ZANZIBAR




Taarifa ilienea sehem tofauti za mji wa Zanzibar:-
Kuna kijana anajulikana kwa jina la Ally mkazi wa Michenzani (Kiswandui)jirani na kwa bi mkubwa stadi umri wake miaka 22 amefariki ghafla maghribi ya leo,taarifa zilopatikana sababu ya kifo chake ni kuwa :-

Alikuwa akicharge simu yake kwa kutumia laptop na wakati huo huo alikuwa anazungumza na mtu kupitia simu hiyo,baada ya cmu kupata joto kali(over heat),simu hiyo ilimripukia na kumuathiri sehemu za mikono,uso hasa upande aloweka simu hiyo na kupelekea kufariki dunia.??? ??? ???? ???? ????? Maziko kesho inshaallah saa 4 msikiti wa Gongoni tafadhali sambaza ujumbe huu kwa wote ili sisi tulio na tabia kama hiyo tuiwache mara moja.Allah amsameh dhambi zake na amuingize peponi kijana Ally 

RIDHIWANI AFANYA KUFURU CHALINZE TAZAMA PICHA

TAZAMA PICHA ZA MGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CCM JIMBO LA CHALINZE ...RIDHIWANI KIKWETE NA NAMNA ANAVYOKUBALIKA




























SHEIKH PONDA ARUDISHWA SEGEREA, OMBI LAKE LATUPWA





Ombi la marejeo lililowasilishwa na Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda limetupiliwa mbali na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilipotoa uamuzi wa pingamizi la awali lililowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), akidai kuwa ombi hilo halikuwa na msingi kisheria. Kesi hiyo iliyosikilizwa kwa saa 1 na dakika 40 ilitolewa uamuzi na Jaji Augustine Mwarija. Baada ya uamuzi huo, Sheikh Ponda alirudishwa jela huko Segerea jijini Dar akiwa chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi.  ilipotoa uamuzi wa pingamizi la awali lililowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), akidai kuwa ombi hilo halikuwa na msingi kisheria. Kesi hiyo iliyosikilizwa kwa saa 1 na dakika 40 ilitolewa uamuzi na Jaji Augustine Mwarija. Baada ya uamuzi huo, Sheikh Ponda alirudishwa jela huko Segerea jijini Dar akiwa chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi. 

Mar 17, 2014

ULIISOMA HII?? DENTI APIGWA RISASI KIFO CHA UTATANISHI


KIFO TATA: DENTI APIGWA RISASI NA KUUAWA…SOMA MKASA KAMILI

MAJONZI, huzuni na masikitiko vimeikumba familia ya Lwena kufuatia mtoto wao mpendwa Dorryce Lwena (27) kufariki dunia kwa kupigwa risasi mkono wa kushoto na ubavu wa kushoto na watu wasiojulikana, Uwazi lilifuatilia.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea mwanzoni mwa mwezi huu, saa tatu usiku, Uwanja wa Edosi, Kitunda, Ilala hatua chache kutoka nyumbani kwa marehemu huyo.
Siku ya tukio, Dorryce ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Singida (DSA), alikuwa akitoka Kariakoo kununua vifaa vya kwenda navyo chuo siku mbili mbele lakini kifo kilimkuta akiwa anakaribia kufika nyumbani.
Kama ilivyo ada, baada ya kujulishwa tukio hilo la kikatili, waandishi wa Uwazi walifika eneo la tukio na kufanya mahojiano na baba wa kufikia wa marehemu ambaye alikuwa akiishi naye baada ya baba mzazi kutengana na mama yake.
Baba huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Maganga alikuwa na haya ya kusema:
“Ilikuwa Jumamosi, Machi Mosi, mwaka huu, saa tatu usiku nikiwa karibu na kwangu, mke wangu (mama wa marehemu) alinipigia simu akaniambia kuna risasi zimepigwa karibu na nyumba yetu, nikamwambia haraka sana wafunge milango na mtu asitoke nje hadi itakapojulikana kuwa risasi hizo zilikuwa za nini.

 “Muda mfupi baada ya kuongea na mke wangu, dada wa Dorryce alinipigia simu akiniambia nirudi nyumbani haraka kwani Dorryce amepigwa risasi na amefariki dunia.
“Nina gari, niliingia ndani yake haraka tayari kwa safari ya kurejea nyumbani. Nikiwa nakaribia nyumbani niliona kundi la watu, nilisogelea eneo hilo na kukuta mwili wa Dorryce umelala katika dimbwi la damu.
“Nilikuta familia yangu, akiwemo mama wa marehemu wakilia kwa uchungu. Iinibidi nikatoe taarifa Kituo Kidogo cha Polisi Kitunda, nao walinishauri niende Kituo cha Polisi Stakishari.


“Polisi walifika eneo la tukio na kufanya michoro kisha wakauchukua mwili hadi Hospitali ya Taifa Muhimbili.
“Mke wangu ana hali mbaya sana jamani. Tangu tukio hilo amekuwa akizimia mara kwa mara, presha inapanda na kushuka. Naombeni msimhoji,” alisema kwa masikitiko makubwa baba huyo.
Alisema mpaka siku hiyo familia ilikuwa haijui chanzo cha mauaji hayo.

Akasema: “Ninachokumbuka mimi siku hiyo mke wangu alimkataza marehemu asiende Kariakoo lakini alikataa, akasema kwa vile Jumapili atakwenda kanisani na Jumatatu ndiyo safari ya kurudi chuo, afadhali aende siku hiyo.”
“Ila wakati marehemu yupo chuoni alizaa na mwanaume mmoja ambaye tulimtaka amhudumie mtoto kwa vile mama yake bado anasoma lakini alikataa, hivyo marehemu aliamua kumchukua mtoto na kumpa. Hadi hapo tukawa hatuna uhusiano naye mzuri,” alisema mzee huyo.
Waandishi wetu walifanya mahojiano na majirani kutaka kusikia kama wanajua lolote juu ya tukio hilo ambapo baadhi yao walisema mauaji hayo hayajawahi kutokea eneo hilo na kudai kwamba marehemu  ndiye anayejua sababu ya kupigwa risasi.
“Marehemu baada ya kupigwa risasi ya kwanza alilia kwa uchungu na kupiga kelele kuomba msaada. Hata hivyo, hakuna aliyejitokeza.
“Aliongezwa risasi ya pili sauti yake haikutokea tena, wale watu walitimka na pikipiki ndipo wananchi tukajitokeza, nahisi ni mapenzi,” alisema mwanamke mmoja anayefanya biashara karibu na eneo la tukio.
Baba mzazi aliyejitambulisha kwa jina la Julius Jacob Lwena anayeishi Tabata Tenge, Dar yeye alikuwa na haya ya kusema:

“Kifo cha Dorryce kimeniuma sana, ila napenda kusema kwamba maisha yake kwa undani siyajui sana kwa sababu nilikuwa mbali naye.
“Mara ya kwanza marehemu alipomaliza elimu ya sekondari alijiunga na Chuo cha Polisi Moshi, alirudishwa kutokana na ujauzito.

“Baada ya kujifungua tulimpeleka Chuo cha Utumishi Singida, bahati mbaya akapata mimba ya mwanaume mwingine, ikabidi arudi nyumbani.
“Baada ya kujifungua tulimpeleka chuo cha uhasibu Singida na mauti yamempata alipokuja likizo,” alisema mzee huyo.

Marehemu alizikwa Machi 4, mwaka huu katika Makaburi ya Tabata Segerea jijini Dar. Mungu ailaze pema peponi roho yake. Amina.
Credit: GPL

Mar 10, 2014

NI MWENDO WA KURUSHANA ROHO; RAY NA CHUCHU VS JOHARI NA OSTAZ JUMA




Johari akipozi na Ostaz Juma Namusoma.
WATU bwana! Picha zilizosambaa mitandaoni zikimuonesha staa wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ akiwa kwenye pozi tata na Ostaz Juma Namusoma zimetafsiriwa kuwa zililenga kuwarusha roho wapendanao; Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hans.


Johari akipozi na Ostaz Juma Namusoma.
Hiyo imekuja baada ya kuvuja habari za Ray kumpangia Chuchu nyumba ya gharama maeneo ya Mwananyamala jijini Dar hivyo Johari ambaye inaaminika kuwa alikuwa mpenzi wa Ray, aliamua kuziachia picha hizo zinazomuonesha akiwa na bosi huyo wa Mtanashati Entertainment ili kumrusha roho Ray.

Ray.
Picha hizo zilisindikizwa na maneno ambayo yalionesha dhahiri kuwa Ostaz ni mtu ambaye amempa Johari msaada mkubwa maishani.
“Huyu (Johari) ni mmoja wa wanawake ambao hatanisahau katika maisha yake, siri ninayo mimi, sijui ninyi mtafikiria nini?” aliandika Ostaz ndipo wachangiaji wakaanza kutiririka:

Chuchu.
“Johari safi sana, kama mbwaimbwai tu, tupia tu picha zozote maana hakuna anayekufunga kama ni huyo Ray, mapenzi yalishakwisha zamani…” mmoja wa mashabiki wake alichangia mtandaoni huku akiungwa mkono na wengine.

Johari.
Paparazi wetu alipounasa mchongo huo, alimvutia waya Johari kumuuliza kama kweli alifanya hivyo kwa nia ya kumrusha roho Ray na Chuchu lakini simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

Chuchu na Ray katika pozi.
Kabla ya penzi hilo motomoto na Chuchu, kwa nyakati tofauti Ray amewahi kuripotiwa kuwa anabanjuka na Johari pamoja na mwigizaji Ruth Suka ‘Mainda’.

UTAJIRI WA KHADIJA SHAIBU “DIDA” WATISHA, KILA MTU ASEMA LAKE…AROBAINI ZAKE ZASUBIRIWA



Toyota Verossa analodaiwa kumiliki Dida.
 AMINI usiamini lakini ndivyo ilivyo! Utajiri wa Mtangazaji wa Radio Times FM ya jijini Dar, Khadija Shaibu ‘Dida’ umeibua gumzo midomoni mwa watu wakidai kuna walakini juu ya upatikanaji wake.
 
Toyota Verossa analodaiwa kumiliki Dida.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Dida ana utajiri mnono lakini anafanya siri ili watu wasiulize alikoupatia kwa sababu si kwa njia halali.
NYUMBA MBILI, MOJA YA GHOROFA
Chanzo kiliendelea kudai kwamba mtangazaji huyo wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani, ana nyumba mbili. Moja ipo Kigamboni na nyingine ipo Goba ambayo ni ya ghorofa  moja, zote jijini Dar.
“Ile ghorofa ya Goba ni kiboko. Ina uwanja mkubwa ndani kama wa mpira, kuna maegesho ya magari hata kumi. Kuanzia getini hadi mlango mkubwa kumesakafiwa,” kilisema chanzo.


Magari aina ya Toyota Carina na Verossa yote mali za Dida yakiwa yamepaki.
MAGARI MATANO YA KUTEMBELEA
Chanzo chetu kikazidi kwenda mbele kwa kudai kuwa mbali na umiliki wa nyumba, pia mwanadada huyo ana magari matano kwa ajili ya kutembelea tu.
“Mbali na nyumba hizo, Dida pia ana magari matano ambayo hubadili anavyotaka kwa ajili ya kutembelea tu kwenye mizunguko yake.

“Ana Toyota Verossa mbili, ana Toyota Noah rangi ya silva na nyeusi. Ana Toyota Vitz. Hivi karibuni ameanza mchakato wa kuingiza nchini gari lingine la sita aina ya Range Rover ‘Vogue’. Hebu fikirieni, Dida huyuhuyu mnayemjua, amepata wapi mali hizo?” kilihoji chanzo.
 
Khadija Shaibu ‘Dida’.
YADAIWA ANAUZA ‘UNGA’
Chanzo kilisonga mbele zaidi kwa kusema kuwa, habari za mitaani ni kwamba mtangazaji huyo anatuhumiwa kuuza madawa ya kulevya ndiyo maana ametajirika ghafla.
“Watu wamekuwa wakimsema kwamba fedha zake zinatokana na biashara ya kuuza unga. Si unajua wauza unga wana pesa sana?” kilisema chanzo hicho.

MADUKA MATATU YA NGUO
Katika tafutafuta, mapaparazi wetu waliwahi kuyanasa maduka matatu ya nguo za kike ambayo yapo Kinondoni, mmiliki wake akiwa ni Dida.
Katika mabango ya matangazo, maduka hayo yanasomeka; Dida Classic.

AMETOKA MBALI
Kabla ya kudaiwa kuwa na utajiri huo, wakati fulani Dida aliwahi kukumbana na misukosuko ya madeni ambapo benki moja maarufu jijini Dar es Salaam ilifilisi samani za sebuleni, nyumbani kwake Kinondoni, Dar baada ya kushindwa kulipa mkopo.

 


Dida akipozi jirani ya gari aina ya Range Rover Vogue alilopanga kulidondosha Bongo.
DIDA ASAKWA
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mapaparazi wetu walimtafuta Dida ili kueleza ukweli ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Mimi sipendi kuanika vitu nilivyonavyo au ninavyomiliki ila ni kweli nina nyumba mbili, moja Kigamboni na nyingine Goba ya gorofa.

KUHUSU MAGARI
“Magari ninayo matatu na si matano, hilo Vogue mchakato unaendelea, ukikamilika nitaliingiza nchini.

MIRADI YA DUKA
“Kuhusu miradi yangu mingine siwezi kuianika hadharani kwa sababu, kwanza sipendi kabisa mambo hayo,” alisema Dida.


Toyota Noah kama anayomiliki Dida.
NI KWELI ANAUZA UNGA?
“Watu wamekuwa wakiongea sana kwamba nauza unga kitu ambacho si kweli, kwanza sijui hata huo unga unafananaje! Ila mimi ninajituma sana kwenye kazi pamoja na kufanya biashara mbalimbali.
“Sitasahau siku ambayo watu walikwenda kutoa taarifa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Dar) kuwa siku hiyo nasafiri na mzigo wa madawa ya kulevya.

“Nilipofika uwanjani nikawekwa chini ya ulinzi na kupekuliwa. Kama haitoshi nilipelekwa Hospitali ya Temeke (Dar) nikafanyiwa X-ray, hawakuona kitu ndipo nikarudishwa uwanja wa ndege kuendelea na safari
“Mimi nawaacha tu waongee watachoka kwa sababu hawajui wanachokifanya, ila mimi najitambua na kile ninachokifanya,” alisema Dida.

Toyota Vitz kama ya Dida.
Akaendelea: “Nilichokuja kubaini ni kwamba kuna wabaya wangu ndiyo walipeleka taarifa za uongo pale uwanjani. Wote huo wivu tu hakuna lingine.
“Kuanzia hapo nikaamua kufanya mambo yangu kimya-kimya, hakuna sababu ya kutangaza kwani wabaya ni wengi, wazuri wachache na si kila anayeku-chekea ni mzuri kwako.”