NYUMBA MBILI, MOJA YA GHOROFA
Chanzo kiliendelea kudai kwamba mtangazaji huyo wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani, ana nyumba mbili. Moja ipo Kigamboni na nyingine ipo Goba ambayo ni ya ghorofa moja, zote jijini Dar.
“Ile ghorofa ya Goba ni kiboko. Ina uwanja mkubwa ndani
Magari aina ya Toyota Carina na Verossa yote mali za Dida yakiwa yamepaki.
MAGARI MATANO YA KUTEMBELEAChanzo chetu kikazidi kwenda mbele kwa kudai kuwa mbali na umiliki wa nyumba, pia mwanadada huyo ana magari matano kwa ajili ya kutembelea tu.
“Mbali na nyumba hizo, Dida pia ana magari matano ambayo hubadili anavyotaka kwa ajili ya kutembelea tu kwenye mizunguko yake.
“Ana Toyota Verossa mbili, ana Toyota Noah rangi ya silva na nyeusi. Ana Toyota Vitz. Hivi karibuni ameanza mchakato wa kuingiza nchini gari lingine la sita aina ya Range Rover ‘Vogue’. Hebu fikirieni, Dida huyuhuyu mnayemjua, amepata wapi
Khadija Shaibu ‘Dida’.
YADAIWA ANAUZA ‘UNGA’Chanzo kilisonga mbele zaidi kwa kusema kuwa, habari za mitaani ni kwamba mtangazaji huyo anatuhumiwa kuuza madawa ya kulevya ndiyo maana ametajirika ghafla.
“Watu wamekuwa wakimsema kwamba fedha zake zinatokana na biashara ya kuuza unga. Si unajua wauza unga wana pesa
MADUKA MATATU YA NGUO
Katika tafutafuta, mapaparazi wetu waliwahi kuyanasa maduka matatu ya nguo za kike ambayo yapo Kinondoni, mmiliki wake akiwa ni Dida.
Katika mabango ya matangazo, maduka hayo yanasomeka; Dida Classic.
AMETOKA MBALI
Kabla ya kudaiwa kuwa na utajiri huo, wakati fulani Dida aliwahi kukumbana na misukosuko ya madeni ambapo benki moja maarufu jijini Dar es Salaam ilifilisi samani za sebuleni, nyumbani kwake Kinondoni, Dar baada ya kushindwa kulipa mkopo.
Dida akipozi jirani ya
gari aina ya Range Rover Vogue alilopanga kulidondosha Bongo.
DIDA ASAKWABaada ya kuzinyaka habari hizo, mapaparazi wetu walimtafuta Dida ili kueleza ukweli ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Mimi sipendi kuanika vitu nilivyonavyo au ninavyomiliki ila ni kweli nina nyumba mbili, moja Kigamboni na nyingine Goba ya gorofa.
KUHUSU MAGARI
“Magari ninayo matatu na si matano,
MIRADI YA DUKA
“Kuhusu miradi yangu mingine siwezi kuianika hadharani kwa sababu, kwanza sipendi kabisa mambo hayo,” alisema Dida.
“Watu wamekuwa wakiongea
“Sitasahau siku ambayo watu walikwenda kutoa taarifa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Dar) kuwa siku hiyo nasafiri na mzigo wa madawa ya kulevya.
“Nilipofika uwanjani nikawekwa chini ya ulinzi na kupekuliwa.
“Mimi nawaacha tu waongee watachoka kwa sababu hawajui wanachokifanya, ila mimi najitambua na kile ninachokifanya,” alisema Dida.
“Kuanzia hapo nikaamua kufanya mambo yangu kimya-kimya, hakuna sababu ya kutangaza kwani wabaya ni wengi, wazuri wachache na si kila anayeku-chekea ni mzuri kwako.”
No comments:
Post a Comment