KIFO TATA: DENTI APIGWA RISASI NA KUUAWA…SOMA MKASA
KAMILI
MAJONZI, huzuni na masikitiko vimeikumba familia ya Lwena kufuatia mtoto wao mpendwa Dorryce Lwena (27) kufariki dunia kwa kupigwa risasi mkono wa kushoto na ubavu wa kushoto na watu wasiojulikana, Uwazi lilifuatilia.
Tukio
Siku ya tukio, Dorryce ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Singida (DSA), alikuwa akitoka Kariakoo kununua vifaa vya kwenda navyo chuo siku mbili mbele lakini kifo kilimkuta akiwa anakaribia kufika nyumbani.
Kama ilivyo ada, baada ya kujulishwa tukio
Baba huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Maganga alikuwa na haya ya kusema:
“Ilikuwa Jumamosi, Machi Mosi, mwaka huu, saa tatu usiku nikiwa karibu na kwangu, mke wangu (mama wa marehemu) alinipigia simu akaniambia kuna risasi zimepigwa karibu na nyumba yetu, nikamwambia haraka sana wafunge milango na mtu asitoke nje hadi itakapojulikana kuwa risasi hizo zilikuwa za nini.
“Muda mfupi baada ya kuongea na mke wangu, dada wa Dorryce alinipigia simu akiniambia nirudi nyumbani haraka kwani Dorryce amepigwa risasi na amefariki dunia.
“Nina gari, niliingia ndani yake haraka tayari kwa safari ya kurejea nyumbani. Nikiwa nakaribia nyumbani niliona kundi la watu, nilisogelea eneo
“Nilikuta familia yangu, akiwemo mama wa marehemu wakilia kwa uchungu. Iinibidi nikatoe taarifa Kituo Kidogo cha Polisi Kitunda, nao walinishauri niende Kituo cha Polisi Stakishari.
“Polisi walifika eneo la tukio na kufanya michoro kisha wakauchukua mwili hadi Hospitali ya Taifa Muhimbili.
“Mke wangu ana hali mbaya
Alisema mpaka siku hiyo familia ilikuwa haijui chanzo cha mauaji hayo.
Akasema: “Ninachokumbuka mimi siku hiyo mke wangu alimkataza marehemu asiende Kariakoo lakini alikataa, akasema kwa vile Jumapili atakwenda kanisani na Jumatatu ndiyo safari ya kurudi chuo, afadhali aende siku hiyo.”
“Ila wakati marehemu yupo chuoni alizaa na mwanaume mmoja ambaye tulimtaka amhudumie mtoto kwa vile mama yake bado anasoma lakini alikataa, hivyo marehemu aliamua kumchukua mtoto na kumpa. Hadi hapo tukawa hatuna uhusiano naye mzuri,” alisema mzee huyo.
Waandishi wetu walifanya mahojiano na majirani kutaka kusikia kama wanajua lolote juu ya tukio
“Marehemu baada ya kupigwa risasi ya kwanza alilia kwa uchungu na kupiga kelele kuomba msaada. Hata hivyo, hakuna aliyejitokeza.
“Aliongezwa risasi ya pili sauti yake haikutokea tena, wale watu walitimka na pikipiki ndipo wananchi tukajitokeza, nahisi ni mapenzi,” alisema mwanamke mmoja anayefanya biashara karibu na eneo la tukio.
Baba mzazi aliyejitambulisha kwa jina la Julius Jacob Lwena anayeishi Tabata Tenge, Dar yeye alikuwa na haya ya kusema:
“Kifo cha Dorryce kimeniuma
“Mara ya kwanza marehemu alipomaliza elimu ya sekondari alijiunga na Chuo cha Polisi Moshi, alirudishwa kutokana na ujauzito.
“Baada ya kujifungua tulimpeleka Chuo cha Utumishi Singida, bahati mbaya akapata mimba ya mwanaume mwingine, ikabidi arudi nyumbani.
“Baada ya kujifungua tulimpeleka chuo cha uhasibu Singida na mauti yamempata alipokuja likizo,” alisema mzee huyo.
Marehemu alizikwa Machi 4, mwaka huu katika Makaburi ya Tabata Segerea jijini Dar. Mungu ailaze pema peponi roho yake. Amina.
Credit:
GPL
No comments:
Post a Comment