Mkuu wa jeshi la polisi
nchinivia Imma Matukio — Jambazi mkuu anayetuhumiwa kujihusisha na matukio ya
mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha yaliyo tokea Wilayani Tarime kuanzia 26
hadi 28.01.2014 amekamatwa na jeshi la polisi jioni ya Tarehe 06.02.2014 mkoani
Tanga.
Akisimulia kukamatwa kwa
jambazi huyo Kamanda wa mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha amesema
kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa jioni ya Tarehe 06.02.2014 majira ya saa 1.30 na
katika mahojiano ya awali ya jeshi la polisi
mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na matukio ya mauaji ya kuanzia tarehe 26 hadi
28 na unyang’anyi wa kutumia silaha pamoja na mengine.
Kamugisha alimtaja
mtuhumiwa huyo kuwa ni Bw. Chaerles Range Kichune, 38 maafuru kama
Josephat Chacha ama Joseph Charles Chacha Msong’o mkazi wa Kenyamanyori kata ya
Turwa Wilayani Tarime.
Aidha Kamugisha amesema
kuwa mtuhumiwa alimtaja Marwa Keryoba Alex 30 – 38 mkazi wa Kijiji cha Kebeyo
Sirari Wilayani kuwa wanashirikiana kufanya ujambazi na silaha ametunzia
nyumbani kwake huko Musoma.
‘“Polisi baada ya kupata
taarifa hizo walifuatilia hadi nyumbani kwa mtuhumiwa ambapo walimkuta na alipo
waona maasikari polisi alijaribu kukimbia huku akiwa amebeba silaha aina ya
(bunduki) SMG .Askari walipiga risasi hewani wakimtaka kujisalimisha lakini
alikaidi na kuanza kuwarushia risasi na ndipo asikari waliendelea kurushiana
risasi na hatimaye kumpiga risasi, marehemu alifia njiani akiwa anapelekwa
hospitalini kwa matibabu,” alisema Kamugisha.
Kamugisha ameendelea
kusimulia kuwa marehemu alikutwa akiwa na Bunduki anina ya SMG moja na iliyo
futwa namba na kukatwa kitako na mtutu,magazine moja na risasi kumi katika
upekuzi nyumbani kwake polisi wamefanikiwa kupata vitu kadhaa vikiwemo simu
mbili za mkononi , CD 21 za picha mbalimbali deki moja,viatu pea mbili na tochi
mbili na mpira wa baiskeli moja na bidha mbalimbali za dukani.
Pia Kamanda alisema
tukio hilo
lilitokea majira ya saa 1.45 Februari 7, 2014 katika Kijiji cha Nyabisare
kata ya Bweri Mjini Musoma mkoani Mara ambapo marehemu ameuawa kutokana na
taarifa zilizo tolewa na Bw Charles Chacha Kichune maafuru (kenonke)
ambaye amemtaja marehemu kuwa ni mshirika wake.
Kamugisha ameshukuru
jeshi la polisi Mkoa wa Tanga kwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi
Tarime/Rorya kuhakikisha jambazi huyo anakamatwa.Pia amewataka wananchi kuwa
watulivu na kuendelea kufanya shuguli zao kama
kawaida wakati hatua zingine zinachukuliwa .
Aidha amewataka wananchi
kutoa ushirikiano na yeyote atakaye toa taarifa ya jambazi kukamatwa atapewa
zawadi ya Tsh milioni moja papo hapo.

No comments:
Post a Comment