Feb 12, 2014

DUDE AFUNGUKA!!! KUWA “WENGI WA MASTAA WA BONGO MUVI WAMETOKEA KATIKA KUJIUZA”



KULWA Kikumba ‘Dude’ amefunguka kuwa wasanii wengi wanaojiingiza kwenye tasnia hiyo wanakuwa ni wadada waliokuwa wakijiuza barabarani kama maeneo ya Baa ya Kimboka iliyopo Buguruni, jijini Dar.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Dude alisema ameshawahi kukutana na wasanii wengi ambao wanataka kujiingiza kwenye tasnia hiyo na wako tayari kutoa miili yao ili waweze kuonekana kwenye runingani.
“Yaani msanii unakuta ameshapata jina lakini alipotokea mpaka kuibuka kisanii utashangaa kabisa na ndiyo maana hata tabia zao huwa zinafanana kabisa na wale wadada wanaojiuza,” alisema Dude.


No comments:

Post a Comment