AMA kweli pombe si maji! Njemba mmoja, Mwala
Kibodi (22) amejikuta akiwa ‘amevurugwa’ na kuzimia mtaroni baada ya
kudaiwa kunywa mizinga minne ya pombe kali aina ya ‘konya’ au ‘ngumu kumeza’.
Mwala Kibodi a.k.a Chegge
akiwa amezimia mtaroni.
Tukio
hilo la aibu lilijiri Sinza-Lion, Dar wikiendi iliyopita ambapo Mwala alikutwa
na wapita njia waliomtambua kuwa ni fundi makenika katika
gereji moja iliyopo maeneo hayo.
Mwala akiingizwa kwenye
bajaji.
Wakiwa
kazini, vijana wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kwa kushirikiana na raia wema,
walianza kumpaka ndimu kama huduma ya kwanza ambapo hakuonesha kuzinduka hivyo
walimpeleka polisi kisha kuchukua fomu ya matibabu (PF3) na kupelekwa Hospitali
ya Sinza-Palestina kwa matibabu.
Akiwa ndani ya bajaj
kupelekwa hospitali.
Akizungumza
na OFM, mmoja wa watu walioshuhudia tukio zima kwa sharti la kutotajwa jina,
alisema Mwala ‘alizima’ kuanzia usiku wa jana yake mishale ya saa mbili mpaka
siku hiyo bila kuzinduka, hali iliyowatia wasiwasi wakihofia huenda mtu huyo
angeweza kupoteza uhai katika maeneo yao.
...Safari ya kuelekea
hospitali.
Akizungumza
na paparazi wetu, rafiki wa karibu wa Mwala, Ramadhan Tito alisema kuwa awali
jamaa huyo alikuwa akibishana na rafiki zake kwamba anaweza kumaliza mizinga
minne ya pombe kali, jambo ambalo wenzake walimbishia.
Mwala akiwa Hospitali ya
Sinza-Palestina kwa matibabu.
Rafiki
huyo alitiririka kuwa kwa kuthibitisha kwamba anao uwezo wa kufanya hivyo,
Mwala alizifakamia pombe hizo kwa sifa hadi kuzimaliza.
Mwala akizidi kupatiwa
matibabu.
Rafiki
huyo alidai kuwa hadi wanaachana na Mwala usiku ule, hakuwa na dalili zozote
kama asingeweza kufika nyumbani kwake, Mabibo, Dar.
Hadi OFM wanaondoka hospitalini hapo,
Hadi OFM wanaondoka hospitalini hapo,







No comments:
Post a Comment