NI
kweli hakuna marefu yasiyokuwa na ncha? Kama ni kweli, basi ile jeuri ya fedha
ya Miss Tanzania
mwaka 2006 ambaye pia hufanya vyema kwenye gemu la sinema za Kibongo, Wema
Isaac Sepetu inadaiwa imefikia nchani....
Kwa
mujibu wa chanzo makini, hali ya kifedha ya staa huyo si nzuri kiasi kwamba kwa
sasa amekuwa mtu wa kushinda ndani kwa kuwa hana mpunga unaomuwezesha kwenda
kujirusha kama zamani.
SABABU
NI NINI HASA?
Chanzo
kilidai kwamba, binadamu aliyekuwa akimmwagia manoti staa huyo aliyetajwa kwa
jina moja la Clement ambaye ni mwajiriwa wa Ikulu jijini Dar, yu hoi kwa kipato
baada ya kunyofolewa kwenye kitengo kilichokuwa na uwezeshaji mwingi wa fedha.
Inadaiwa
kuwa, baada ya Clement ambaye ni mume wa mtu, kuondolewa kwenye kitengo hicho
amepelekwa sehemu nyingine ambayo mchana kutwa ni kupiga miayo mpaka muda wa
kutoka kazini.
MKONO
WA MKEWE WATAJWA
Katika
madai hayo, inasemekana mke wa Clement (jina tunalo) ana mkono wa kile
kilichompata mumewe, kuondolewa kwenye kitengo chenye ulaji na pia amekuwa
akiwawinda wawili hao ili awafanyie fumanizi kwa sababu Clement ni mumewe wa ndoa.
KILICHOTOKEA
SASA
Chanzo
kikaendelea: “Baada ya kuondolewa kwenye sehemu yenye fedha na kutupwa kwenye
ukame, jamaa akaanza kupata tabu kwani fedha alizokuwa akimpa Wema zamani
zikawa hazipo.
“Hilo likamwathiri na Wema
mwenyewe kwani ile jeuri mliyokuwa mnamuona nayo akiifanya kwa rungu la fedha,
mara sherehe, mara kumlipia Kajala (Masanja) makahamani (Kisutu), mara kwenda
baa na wapambe imekatika ghafla.
“Siku
hizi Wema ndani na yeye, yeye na ndani. Naamini hata mkienda kwake muda huu
(juzi Jumatatu saa 5 asubuhi) mtamkuta.”
INADAIWA
AMEUZA MAGARI MAWILI
Habari
zaidi kutoka chanzo hicho, hali ilipozidi kubana sana , Wema aliamua kuuza magari mawili kati
ya matatu anayomiliki ili apate fedha za kuendelea kujikimu katika maisha ya
kila siku.
Magari
hayo mawili yanasemekana ni Toyota Mark II GX 110 na Toyota Harrier na kubakiwa na Audi Q7.
YALIYOMPATA
CLEMENT
Habari
zinazidi kudai kwamba hali ikazidi kuwa mbaya kwa Clement kiasi kwamba
alijikuta akikabwa koo na benki moja ya jijini Dar es Salaam ambayo aliiomba
mkopo wa Shilingi mil. 120 akitumia hati ya nyumba ambayo pia si yake.
Benki
hiyo ilipozidi kumbana, mkewe (sasa wametengana) ambaye naye anadaiwa kuwa
‘mzuri’ kwenye fedha alikwenda kulipa fedha hizo benki ili nyumba ya watu
isinadiwe na benki hiyo iliyokuwa haitaki mambo ya utani kwenye
marejesho.
Madai
mengine ambayo hayajathibitishwa yanasema kuwa, mtikisiko huo wa kifedha kwa
Clement umesababisha awe ‘choka mbaya’ kiasi cha sasa kuanza kupiga mizinga kwa
rafiki zake.
WEMA
ASAKWA ASEME UKWELI WAKE
Baada
ya kupokea ishu hiyo, Risasi Mchanganyiko liliamua kumsaka Wema ili aseme
lolote kuhusiana na tuhuma hizo.
Saa
4:32 Wema alipigiwa simu yake ya mkononi ambayo iliita kwa muda mrefu bila
kupokelewa hata pale iliporudiwa tena na tena.
Baada
ya jitihada hizo kugonga mwamba, Risasi liliamua kumwendea hewani meneja
wake Martin Kadinda ambaye naye hakupokea simu licha ya kupigiwa zaidi ya mara
tatu.
Risasi
Mchanganyiko halikukata tamaa, kwani ni haki ya msingi kwa Wema kuongelea suala
hilo .
Likampigia msaidizi wake wa karibu anayeitwa Pat Man, yeye alipokea, akaulizwa
kuhusu bosi wake huyo, akasema:
“Wema
anaumwa (hakutaja ugonjwa), ametoka hospitali sasa hivi (hakusema
hospitali gani) yuko nyumbani.”
Waandishi
wetu wakafunga safari hadi nyumbani kwa Wema - Makumbusho (lakini ni
Kijitonyama).
Getini
alikutwa mlinzi mahiri kwa mwonekano ambapo alipoombwa kumwita Wema au
kumwambia kuna waandishi wapo nje, alisema:
“Mh!
Kwa kweli si rahisi kutoka, amelala anaumwa... alikwenda hospitali amerudi muda
si mrefu.”
Alipochombezwa
kwa maneno ya ‘kisiasa’ kwamba awaambie wasaidizi wake wa ndani wakamwamshe,
alikataa akisema litazuka timbwili ambalo yeye hakuwa tayari kuliona.
“Bosi
akilala huwa hapendi kuamshwa, hasa kama hayuko
sawa. Watu wanaomwamsha ni wale wenye ahadi naye,” alisema mlinzi huyo.
WEMA
ATUMIWA MESEJI
Baada
ya kuondoka nyumbani kwa Wema, Risasi Mchanganyiko lilimtumia ujumbe mfupi
(SMS) ‘mreeefu’ wenye madai yote na ikaonesha ‘delivered’ kwenye simu ya Wema,
lakini pia haikujibiwa.
TUNARUDI
KWA CLEMENT
Simu
yake haikuwa ikipatikana hewani alipopigiwa ili na yeye apewe nafasi ya kusema
lolote kuhusu sakata hilo .
MKE
WA CLEMENT AVUNJA UKIMYA
Risasi
Mchanganyiko liliamua kumsaka kwa simu ya mkononi mke wa Clement ambapo
alipopokea na kusomewa mashitaka ya mumewe na nafasi yake kama
shahidi muhimu alikiri hali ya jamaa kuwa tete kimfuko.
“Kuhusu
hilo la nyumba
ni kweli ilikuwa inadaiwa na benki (aliitaja jina) na walitaka kuinadi ili
wapate fedha zao, lakini nikaingilia kati ili kulinda heshima ya familia.
“Unajua
ile nyumba kuna mtu alituuzia, kwa hiyo Clement alitoa kiasi cha fedha lakini
hakumalizia na akatumia hati ya nyumba kwenda kuombea huo mkopo. Kwa sababu
benki walikuja juu nilitafuta mtu akainunua, kiasi cha fedha nikammalizia
aliyetuuzia na kulipa benki,” alisema mwanamke huyo.
KUHUSU
KUMFANYIA FITINA MUME AKAHAMISHWA KITENGO
Huyu
hapa mke wa Clement: “Hilo
si kweli bwana. Kwanza mimi ndiyo nilimfikisha
pale alipofika. Sasa mtu nimuinue mwenyewe nitamfanyiaje fitina?
“Kwanza mimi siko naye siku hizi. Nilipoona anachukua
magari ya nyumbani na kuyapeleka huko kwa nani sijui (Wema) nikaamua kukaa
pembeni na kunyamaza kimya.
“Kama ni mabalaa anayapata hukohuko aliko, nisisingiziwe
mimi kwa lolote lile.”
KUHUSU
KUMWANDALIA FUMANIZI WEMA
“Aaa
wapi! Nimwandalie fumanizi la nini? Yeye ana maisha yake mengine mimi niko na
mambo yangu, muda huo sina kabisa, yaani niko bize sana ,” alisema mwanamke huyo huku akidai muda
huo alikuwa akidraivu.
Source: Gazeti la Risasi/ Global publisher.
Source: Gazeti la Risasi/ Global publisher.
No comments:
Post a Comment