NYOTA wa filamu na mshindi wa
zamani wa Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike nchini, Riyama Ally a.k.a Riyama
amewataka wasanii wenzake kuacha tabia alizoziita za kijinga kwa kuiga maisha
na uigizaji wa wasanii wa ng’ambo.
Riyama ambaye sifa yake kubwa
kwenye ‘game’ ni kuvaa uhusika, hasa wa kumwaga machozi, alisema hayo hivi
karibuni katika mahojiano maalum na gazeti hili jijini Dar es
Salaam .
“Usanii si kukaa uchi, unajua baadhi ya wasanii wenzetu wanashindwa kufahamuhilo . Kukaa
uchi hakumaanishi ndiyo utaonekana mzuri zaidi,” alisema kwa masikitiko
Riyama.
Akizidi kushusha ‘maskadi’ Riyama alisema, tatizo kubwa walilonalo wasanii wa Kibongo ni kuiga, mwenyewe anafafanua: “Haijakatazwa kuiga, lakini unatakiwa kujua unaiga nini. Hatuwezi kuchukua tamaduni za watu na kuleta kwetu. Wao wana miiko yao, nasi pia. Kwanini tuige ujinga?”
Alisema, wasanii kuvaa nguo fupi zisizo na heshima, huua soko la filamu bila la wasanii wenyewe kujua kwani watu wenye heshima zao hawawezi kununua na kwenda nazo majumbani mwao
“Usanii si kukaa uchi, unajua baadhi ya wasanii wenzetu wanashindwa kufahamu
Akizidi kushusha ‘maskadi’ Riyama alisema, tatizo kubwa walilonalo wasanii wa Kibongo ni kuiga, mwenyewe anafafanua: “Haijakatazwa kuiga, lakini unatakiwa kujua unaiga nini. Hatuwezi kuchukua tamaduni za watu na kuleta kwetu. Wao wana miiko yao, nasi pia. Kwanini tuige ujinga?”
Alisema, wasanii kuvaa nguo fupi zisizo na heshima, huua soko la filamu bila la wasanii wenyewe kujua kwani watu wenye heshima zao hawawezi kununua na kwenda nazo majumbani mwao
No comments:
Post a Comment