SINEMA
ya madai mazito dhidi ya mastaa wa filamu
Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’, Ruth Suka ‘Mainda’ na Chuchu Hans ambaye ni
mke wa mtangazaji Frank Mtao kuchanganywa kimapenzi na Vincent Kigosi ‘Ray’
sasa inaendelea na mhusika mkuu Ray amefunguka na kueleza yake ya moyoni huku
akisisitiza: “Chuchu ndiye mke wangu, tarajieni makubwa soon (hivi karibuni).”
Akizungumza wikiendi
iliyopita katika Viwanja vya TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam ambapo
kulikuwa na mechi kati ya wasanii wa Bongo Fleva na Bongo Muvi, Ray
aliwashangaa waandishi kwa kumshambulia kutoka kimapenzi na Chuchu.
Mwandishi alianza kwa kumwuliza: “Ray magazeti yanaandika kuhusu wewe kutoka na Chuchu Hans ambaye ni mke wa mtu. Mainda amezungumza mengi. Kukaa kwako kimya bila kufafanua chochote siyo kitu kizuri. Tafadhali, hebu zungumza japo kidogo kuhusu madai ya Mainda.”
RAY: Sikia nikuambie, huyo Mainda utoto unamsumbua. Haniumizi kichwa kabisa. Kuhusu Chuchu... si mmeshaandika? Endeleeni kuandika lakini soon mtashuhudia kitu kikubwasana .
RISASI: Ni kitu gani hicho?
RAY: Niacheni na Chuchu wangu.... kifupi ndiye mke wangu na itawashangaza wengi. Halafu mimi nawashangaasana .
Yaani mimi kutoka na Chuchu mnakuzaaaa... mbona alivyokuwa na ma-boyfriend zake
wengine hamkuandika? Kwa sababu ni Ray basi mkaona ni habari. Mimi ninavyojua
Chuchu siyo mke wa mtu.
Kwanza mimi sijamchukua kutoka mikononi mwa mumewekama
mnavyosema. Chuchu tayari alikuwa na maisha yake mapya. Nilimchukua kutoka kwa
Libert (hajafafanua zaidi ni nani). Mbona alivyokuwa na huyo Libert
hamkuandika? Kifupi niacheni na maisha yangu.
RISASI:Vipi kuhusu Johari?
RAY: (Huku akikimbia kuingia uwanjani) Tena huyo mama yako (akimuonesha mwandishi Johari) anakuja.
Mwandishi wetu aliachana na Ray aliyekuwa akiingia uwanjani na kumfuata Johari lakini hakuwa tayari kusema chochote achilia mbali hata kumsikiliza mwandishi wetu!
TUJIKUMBUSHE
Hivi karibuni gazeti hili liliandika habari yenye kichwa MAINDA: NIMETOA MIMBA YA RAY. Ndani yake Mainda alifunguka mengi ikiwemo kuchanganywa kimapenzi na Ray, yeye na wenzake Johari na Chuchu Hans.
Mwandishi alianza kwa kumwuliza: “Ray magazeti yanaandika kuhusu wewe kutoka na Chuchu Hans ambaye ni mke wa mtu. Mainda amezungumza mengi. Kukaa kwako kimya bila kufafanua chochote siyo kitu kizuri. Tafadhali, hebu zungumza japo kidogo kuhusu madai ya Mainda.”
RAY: Sikia nikuambie, huyo Mainda utoto unamsumbua. Haniumizi kichwa kabisa. Kuhusu Chuchu... si mmeshaandika? Endeleeni kuandika lakini soon mtashuhudia kitu kikubwa
RISASI: Ni kitu gani hicho?
RAY: Niacheni na Chuchu wangu.... kifupi ndiye mke wangu na itawashangaza wengi. Halafu mimi nawashangaa
Kwanza mimi sijamchukua kutoka mikononi mwa mumewe
RISASI:Vipi kuhusu Johari?
RAY: (Huku akikimbia kuingia uwanjani) Tena huyo mama yako (akimuonesha mwandishi Johari) anakuja.
Mwandishi wetu aliachana na Ray aliyekuwa akiingia uwanjani na kumfuata Johari lakini hakuwa tayari kusema chochote achilia mbali hata kumsikiliza mwandishi wetu!
TUJIKUMBUSHE
Hivi karibuni gazeti hili liliandika habari yenye kichwa MAINDA: NIMETOA MIMBA YA RAY. Ndani yake Mainda alifunguka mengi ikiwemo kuchanganywa kimapenzi na Ray, yeye na wenzake Johari na Chuchu Hans.

No comments:
Post a Comment