Seneta Mike Sonko wa Nairobi , Kenya
ni miongoni mwa watu wasiopotea katika vichwa vya habari vya mitandao ya Kenya , huenda
sababu ni moja, ana matukio ya kutengeneza ‘attention’ hasa yale ambayo wengi
wanaamini hayaendani na kofia ya ‘useneta’ aliyoivaa.
Ukiachana na mitindo yake ya
kunyoa nywele (kiduku), huku kichwani kukiwa na urembo wa maandishi kama
wafanyavyo wasanii au wachezaji wa mpira,
Seneta huyo huwa ni mtu wa kupiga
pamba na bling bling shingoni, masikioni na vidole vyake huchafuliwa na gold,
kuna uwezekano akisimama na Octopizzo unaweza ukahisi Sonko ndiye msanii na
Octo ni dereva wake. (Joke)Mtandao wa Nairobi
Wire umeweka picha ya simu ya mezani inayotumika katika ofisi ya Seneta huyo wa
Nairobi , yenye
mfano wa umbo la msichana aliyevaa bikini pamoja na bra zenye bendera ya
Uingereza. Katika picha hiyo Sonko anaonekana akiongea
kupitia simu hiyo.
kupitia simu hiyo.




No comments:
Post a Comment