Naaam Mswahili mwenzangu, leo
japo kiduchu nimeona poa tuzungumze kuhusu tabia za akina mama wa mujini hasa
wale ambao ni mambo safi wene tabia ya kuchukua
wasichaa toka shamba na kuwaweka ndani kama ‘ma
hausi geri’
Akina mama hao wamekuwa
wakijisahau kiasi chakumpa mtumishi huyo majukumu yenye kuashiria kupitiliza.
Utamkuta msichana wa kazi ndiye mpishi wa chakula cha baba siku zote, yeye
ndiye anayemuandalia baba maji ya kuoga na mambo yanapozidiana msichana wa kazi
hutakiwa hata kufagia na kuipamba chumba cha wazee.
SASA JIULIZE??? KAMA WEWE NI
MWANAMUME MKEO HAFANYI MAJUKUMU YOOTE HAYO NA YANAFANYWA NA DADA WA KAZI NA
ANAYAFANYA VIZURI KIASI CHA KUKURIDHISHA, KWA NINI USIMPE KIBALI CHA KUWA BI
MDOGO????
Domo la Mswahili

No comments:
Post a Comment