‘We Talking Money You Talking
Nonsense’ huenda ikawa kauli nzuri kuelezea hiki walichokifanya P-Square kwa
sasa.
Hakuna ubishi kuwa, kwa
hiki walichokifanya sasa, na kama macho yetu
hayatudanganyi kwa hiki yanayokiona, mapacha hawa wamefanya kufuru. Kama hii inayoonekana ni dhahabu kweli, basi P-Square,
hela wanayo.
Peter ameshare picha hizi nne ambazo
wiki hii zitakuwa gumzo barani Afrika ambapo kwenye picha moja inayomuonesha
pacha mwezie Paul akiwa amesimama kwenye sebule mpya inayoaminika kuwa ya
nyumba yao
mpya, ameandika ‘Goldenworld #blessed.’
Kwenye picha nyingine, wanaoonekana
wakiwa pamoja kwenye sebule hiyo iliyotawaliwa na kile kinachoonekana kama dhahabu zilizozunguka sofa za kuvutia na Peter
ameandika: #2kings…… Work hard,play harder.’
Picha nyingine inamuonesha Peter akiwa
peke yake kwenye meza ya chakula, kubwa, iliyojaa vyombo vya thamani vya
kuvutia na ameandika: A king in my own world…. #Blessed.”





No comments:
Post a Comment