Dec 22, 2013

CHADEMA KULIKONI???

 

Ewe Mswahili mwenzangu mara bada ya kuisoma hotuba ya Zitto Kabwe, Kigoma, aliyoitoa jana, nimebaki na kitu ninachokiona; kuwa sasa kuna Chadema mbili mpaka pale wenye kuvutana ndani ya Chadema watakapotuhakikishia kwa vitendo kuwa kuna Chadema moja. Maana kwa kuyasoma haya ya Zito; "Mabadiliko ni kiu kikubwa cha Tanzania kwa sababu mabadiliko huleta matumaini. Na kiu hii ni kubwa zaidi kwetu sisi vijana wa kizazi hiki kipya. Siasa za kizazi kipya cha viongozi ni siasa za majawabu ya kero za wananchi. Siasa za mabadiliko ni siasa za kujenga na kuimarisha; ni siasa za kuaminiana na kuheshimiana hata pale mnapopingana kimawazo. Ninataka tujenge siasa mpya Tanzania;siasa za mabadiliko; siasa zinazojenga matumaini ya kweli;siasa zinazowajali na kuwajengea uwezo wananchi wa Tanzania." - Zitto Kabwe.
Naam, Kwa kuyasoma hayo, sasa naziona ' Chadema Mabadiliko', au labda 'Chadema - Mageuzi' na ' Chadema- Asilia'. Naendelea kutafakari.
Chanzo ni: Maggid Mjengwa,
Bagamoyo.


No comments:

Post a Comment