MWILI wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Balozi Fulgence Kazaura umewasili jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifaa wa Julius Nyerere ukitokea nchini India alipofia wakati akipatiwa matibabu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick aliongoza shughuli zote za kupokea mwili wa Balozi Kazaura katika uwanja wa ndege.
Mwili wa marehemu Kazaura unatarajiwa kuanza kuagwa leo jijini Dar kabla ya kusafirishwa siku ya Ijumaa kwenda mkoani Kagera kwa maziko yatakayofanyika Jumamosi.
HISTORIA FUPI
Marehemu Kazaura aliteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mkuu wa Chuo Kikuuu cha Dar es Salaam mwaka 2011 kwa kipindi kingine cha miaka minne baada ya kumaliza kipindi kama hicho.
Mwanzoni marehemu aliteuliwa na Rais Kikwete kushika nafasi hiyo baada ya kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Chuo hicho, Paul Bomani kufariki dunia baada ya kuongoza tangu mwaka 1993 hadi alipofariki dunia mwaka 2005.
No comments:
Post a Comment