ZAIDI ya kilo
200 za madawa ya kulevya aina ya Heroin yamekamatwa na kikosi cha polisi
wanamaji katika Bahari ya Hindi yakisafirishwa kutokea nchini Irani pamoja na
mabaharia kumi na wawili kutoka nchi ya Irani na Pakistani.
Kamanda wa
polisi kikosi cha wanamaji Mboje Kanga ameeleza kuwa tukio hilo lililotokea
usiku wa tarehe 4 majira ya saa sita usiku ambapo waliweza kukamata jahazi hilo
na mabaharia kumi na mbili wote wakiwa hawaijui lugha ya Kiswahili wala
Kingereza na jahazi lao halikuwa na utambulisho wowote wa sheria za majini.
Mkuu wa
kitengo cha kudhibiti dawa za kulevya, Godfrey Nzowa amesema jahazi hilo
liliweza kukamatwa baada ya kikosi cha polisi cha wanamaji kuendelea na
operesheni zake za doria majini na mara baada ya kulitilia shaka waliweza
kulikamata na baada ya kulikagua walikamata shehena hiyo ya madawa ya kulevya
aliyoyataja kuwa ni aina ya Heroin ambayo mengi huzalishwa nchini.
No comments:
Post a Comment