UMRI
HALISI WA CELEBRITIES WA KIBONGO
Kwa nini hawa wanao itwa " celebrities "
wa kibongo wanapenda kupunguza miaka yao ?.
Kisa nini? au ndio waonekane ni watoto wa dogo ambao wanafanya mambo makubwa?.
Leo ninatoa miaka ya kuzaliwa ya baadhi ya celebrities wa kibongo vis miaka
wanayo dai kuwa nayo.
SASA
NAKUJA KWA CELEBRITIES WA KIBONGO:
JUMA KASEJA...Anadai amezaliwa
mwaka 1985. Mwaka 2000 alikuwa kipa namba moja wa timu ya Moro United, which
means kwamba ameanza kucheza Ligi kuu Tz akiwa na miaka 14/15 ?
Kwa
muonekano wake na rekodi zake, Juma Kaseja amezaliwa kati ya mwaka 1976 -1980.
BAMBO ( Mchekeshaji ): Miezi
kadhaa kwenye kipindi cha watoto wetu cha ITV alisema amezaliwa mwaka 1985..
Nimeanza kumuona Bambo kwenye maigizo ya Kaole ITV mnamo mwaka 2000 ambapo
alikuwa anaonekana mwanaume mwenye zaidi miaka 25. Kipindi Bambo alikuwa
anaigiza kama Mganga wa kienyeji, na alikuwa
akimtaka Nyamayao (kipindi hicho yeye pamoja na Kibakuli walikuwa na miaka 15 )
Kama Bambo anachosema ni kweli maana yake ni
kwamba, mwaka 2000 wakati akiigiza Kaole kama
Mganga wa kienyeji, alikuwa na umri wa miaka 15. Sio kweli.
Bambo atakuwa amezaliwa kati ya mwaka 1972 na
1976....
WEMA SEPETU : Mwaka jana kwenye
BDAY ya Wema Sepetu, aliyekuwa msanii Diamond aliandika kwenye ukurasa wake wa
face book, twitter na blogu yake HBD WISHES kwa wema akisema " HONGERA KWA
KUFIKISHA MIAKA 22 ". Kama Diamond alikuwa sahihi, ina maana Wema Sepetu
alizaliwa mwaka 1990, kitu ambacho sio sahihi kwa sababu zifuatazo ;
Wema Sepetu alitwaa taji la Miss Tz mwaka 2006.
Under 18 hawaruhusiwi kushiriki shindano hili, hii ina maana wema slishiriki
miss tz akiwa na miaka 16? no way?. Mnamo mwaka
2006 wema alinukuliwa na media mbalimbali akisema amezaliwa mwaka 1988( I ALSO
DOUBT THIS ).( So miaka ya wema inabadilika kama
matokeo ya kwenye cheti cha mwanafunzi anaye risiti mtihani au cheti cha angaza
cha mzinzi ?) Wema Sepetu amezaliwa kati ya mwaka 1985 -
1986.
LE Mutuz anaficha umri wake na
ana jaribu kujustify kwamba yeye bado serengeti boy kwa ku behave immaturely.
Chanzo makini kinatueleza ya kwamba, LE MUTUZ alizaliwa mnamo tarehe 16 DESEMBA
1961, na baba yake alimpa jina la UHURU.
Diamond anasema amezaliwa mwaka
1989, lakini chanzo cha kuaminika kinasema, Diamond amezaliwa mwaka 1986.
MwanaFA anasema amezaliwa mwaka
1980. Chanzo cha kuaminika ( TENA SANA )kinasema mwana FA amezaliwa mwaka 1974.







No comments:
Post a Comment