Mwanamuziki na muigizaji baby Joseph madaha
amefunguka na kusema kuwa kweli ameamini uchawi na kupigana juju vipo kwenye
gemu kwani mambo yaliyomtokea hivi karibuni haelewi hata imekauje.
Chanzo nini?
Hapo siku za nyuma baby
Madaha alipatikana na dhahama ya kukumbwa na kashfa nzito sana ya kujiuza kwa
dau la milioni kumi kwa jamaa mmoja hivi mitaa ya Dar es Salaam Jambo lilolopelekea
yeye kupigwa chini na Record label yake ya Candy and Candy ya huko Kenya na
kupokonywa gari aina ya AUDI TT aliyokuwa akitembelea huku akiharibu pia
uhusiano wake na bosi wa record label hiyo – Joe kairuki ambaye pia anadaiwa
kuwa mpenzi wake.
Je ni Kweli alijiuza?
Baby Madaha ambaye
amerudi nchini hivi karibuni tokea Nairobi
alipoenda “ku-solve” ishu yake hiyo na label hiyo anasema yani hata haelewi
kitu gani kilitokea siku hiyo ingawa mpaka akaandikwa kama
alienda kujiuza, anachokumbuka ni kupigiwa simu na mtu asiyemfahamu an
kumwambia anataka wafanye naye kazi ya kusambaza filamu yake mpya ya Gal
Bladder ambaye inatikisa soko kwa sasa.
Baada ya kufika hapo
waliongea vizuri na kuondoka ghafla kabla ya kuja kusoma kesho yake kuwa
alikuwa anajiuza kitu ambacho ansema hajui kimetoka wapi.
“Yani hata sielewi
ilikuaje nikaenda kukutana na yule jamaa, ilikuwa ni kama muujiza hivi, mwanzo
nilisita sana ila nikashangaa nimefika tu pale
bila kujielewa, ni vitu vya ajabu sana ”
alieleza baby Madaha.
Uhusiano wake na Label
hiyo ukoje sasa?
Akizungumza na
bongomovies, baby amesema kwa sasa kila kitu kipo sawa kwani alipoenda Kenya
waliongea vizuri na bosi wake huyo na kumaliza tofauti zao na sasa amerudi
nchini kusambaza filamu yake hiyo mpya ya Gal bladder huku akijiindaa kupiga
show kwenye tour yake aliyoiandaa jina la Top Up and Refill
itakayofanyika mwezi ujao wa tatu.
Mwenyewe anasemaje
zaidi?
Hata wafanyaje,
waniroge, wanichafue, i’m a bad gal, na sibabaishi na vijimaneno vya watu hata
kidogo, sitoki candy and Candy hata waloge kwa waganga wote duniani. Kama
walifikiri nimeumbuka, wajue watasubiri sana .
Nikitoka kenya
naenda Holywood tu!


No comments:
Post a Comment