Picha
hii ni ya maktaba ( si ya tukio la jana )
BASI la Zuberi lenye namba T119 AA2 limepata ajali mbaya katika kijiji cha Nkuhi wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida na watu wanne wameripotiwa kufa papo hapo kwa kukatwa vichwa huku majeruhi wengi wakiwa wameumia vibaya sehemu mbalimbali za mwili.

Akizungumza kutoka eneo la tukio leo
mchana huu, mwandishi wa habari, Nathanieli Limu amesema basi hilo la Zuberi lilikuwa
linatoka Mwanza kuja Dar na lilikuwa na zaidi ya abiria 60.
Amesema kuwa chanzo cha ajali ni dereva
wa basi hilo
ambaye alikuwa anajaribu kumkwepa bibi kizee aliyekuwa anakatisha
barabarani kwenye majira ya saa saba mchana.
“ilikuwa si ajali ya kawaida baada ya
bibi kizee kukatiza barabarani na wakati dereva anajaribu kumkwepa alirudi mara
ya pili barabarani ndipo hapo gari lilipinduka na kuanguka kwenye mtaro,”
amesema Limu
Alilisitiza kwamba mashuhuda wa ajali
hiyo wanahusisha tukio hilo
na imani za kishirikiana baada ya bibi huyo kuamua kurudi mara ya pili
barabarani na kusababisha ajali na kukaa kwa muda mrefu eneo la tukio.
Amesema kuwa basi hilo
la Zuberi liliinuliwa na lori lenye kifaa maalumu cha winch baada ya basi hilo kumlalia mtoto mdogo
wa miezi kadhaa ambaye mama yake ni miongoni mwa waliofariki dunia papo hapo na
maiti yake kupelekwa hospitali ya mkoa wa Singida.
SHUKA
CHINI KUTOA MAONI YAKO

No comments:
Post a Comment