Utangulizi
Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa sugu ambao huathiri njia za hewa ambazo huingiza na kutoa hewa katika mapafu. Upatapo ugonjwa wa pumu, kuta za ndani za njia ya hewa hupata maumivu (inflammation) na kuvimba.
Maumivu katika njia za hewa huzifanya kujihami kwa kusinyaa na hivyo kupunguza kiasi cha hewa kinachopita kwenda kwenye mapafu. Hali hii husababisha muathirika kutoa mliokama wa filimbi au mluzi
wakati wa kupumua.
Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa sugu lakini unaotibika. Unaweza kudhibitiwakama vile ugonjwa wa kisukari na moyo unavyoweza
kudhibitiwa.
Aina za Pumu
Kuna aina kuu mbili za pumu. Aina ya kwanza ni ile inayoanza mapema (early onset asthma) na aina ya pili ni ile inayochelewa kuanza (late onset asthma).
Kwa kifupi tutaenda kuangalia tofauti chache kati ya aina hizi za pumu.
Pumu inayoanza mapema
Ni kawaida kwa aina hii ya pumu kuanza utotoni na kwa kawaida huwatokea waathirika ambao miiliyao
hutengeneza kingamwili (antibodies) za IgE.
Waathirika wa aina hii ya pumu hutambuliwa kwa vipimo maalum vya ngozi ambapo huonesha kuathirika kwa asilimia kubwa vipimo hivyo vinapofanywa.
Pia waathirika hawa huwa na matatizo mengine ya mzio (allergic disorders)kama mafua na ukurutu (eczema).
Pumu inayochelewa kuanza
Aina hii ya pumu tofauti na iliyopita huanza katika umri wowote na asilimia kubwa ya waathirika ni watu wazima. Hakuna ushahidi wowote unaohusianisha vizio (allergens) vinavyotokana na mazingira na uwezo wa kusababisha aina hii ya pumu.
Pumu husababishwa na nini?
Bila shaka mpenzi msomaji umekua ukijiuliza swali hili mara kwa mara. Haifahamiki haswa ni sababu zipi zinazopelekea njia za hewa kupata maumivu na hivyo kupelekea mtu kupata pumu.
Vyanzo mbali mbali vinaonyesha kuwa inatokana na mseto wa vitukama tumbaku, maradhi na baadhi ya vizio.
Pia kuna vitu katika mazingira ambavyo vinaweza kusababisha mtu kushambuliwa na pumu. Vitu kama vile mazoezi, vizio, viwasho (irritants) na maradhi yatokanayo na virusi.
Baadhi ya vizio ni kama vifuatavyo:
-Vumbi
-Mende
-Chavua (pollen) kutoka kwenye miti na majani
-Magamba ya wanyama, manyoya n.k
Viwasho kama:
-Moshi wa sigara
-Uchafuzi wa hewa
-Harufu kali (kutoka kwenye rangi au chakula)
-Msongo wa mawazo
Vingine ni kama:
-Dawa kama Aspirin
-Ugonjwa wa kucheua
-Viwasho au vizio vitokanavyo na kemikali
-Magonjwa ya njia ya hewa n.k
Ieleweke kwamba orodha iliyotajwa hapo juu siyo kamilifu kwa maana kwamba haijasheheni vitu vyote vinavyoweza kuleta dalili za pumu na pia muathirika anaweza kuathirika na kimoja wapo au zaidi.
Vigezo hatarishi
Baadhi ya vigezo hatarishi vinavyoweza kuongeza uwezekano wa kusababisha ugonjwa wa pumu ni pamoja na:
-Kuishi katika miji mikubwa, haswa katikati ya mji ambapo huongeza uwezekano wa kukutana na vizio
-Kuvuta hewa iliyo na moshi
-Kemikali zitokanazo na kilimo, dawa za kutengeneza nywele, rangi, vyuma, plastiki au vifaa vya elektroniki
-Kuwa na mzazi mmoja au wawili wenye pumu
-Kuathirika na maradhi ya mfumo wa hewa kama kikohozi na mafua wakati wa utoto.
-Unene wa kupita kiasi (obesity)
-Ugonjwa wa kucheua na kiungulia (Gastro esophageal reflux disease)
Dalili za Pumu
Baadhi ya dalili za kawaida za ugonjwa wa pumu ni kama zifuatazo:
-Kikohozi: Mara nyingi kikohozi cha pumu huwa kikali nyakati za usiku au alfajiri na hivyo kumfanya mwathirika kutolala vizuri
-Kutoa sauti ya mfano wa mtu anayepiga mluzi au filimbi wakati wa kupumua
-Kifua kubana: Mgonjwa husikia kama kitu kinakandamiza kifuani au wakati mwingine husikia kama mtu amemkalia kifuani.
-Kukosa hewa: Baadhi hujisikiakama hawawezi
kupumua na kukosa hewa ya kutosha inayoingia au kutoka kwenye mapafu.
-Kupumua haraka haraka
Ikumbukwe kwamba si watu wote huwa na dalili zilizokwisha tajwa hapo juu na dalili zaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu.
Dalili pia zinatofautiana ukali. Wakati kwa mwingine dalili zinakuwa za wastani, wengine zinakuwa za kukera tu au mbaya kiasi cha kumzuia muathirika kufanya shughuli zake za kila siku.
Vile vile wapo wengine ambao dalili zinakuwa mbaya kiasi cha kuhatarisha maisha. Dalili pia zaweza kutofautiana kwa kipindi zinapotokea.
Wengine hupata dalili mara moja tu kwa mwezi, wengine kila wiki na wengine hupata dalili kila siku.
Hata hivyo iwapo muathirika atapata matibabu sahihi anaweza kuishi na dalili chache au bila dalili kabisa.
Uchunguzi
Kipimo cha muhimu katika uchunguzi iwapo mtu ameathirika na pumu ni kuangalia jinsi mapafu yanavyofanya kazi.
Kipimo hicho kijulikanacho kwa lugha ya kitaalamukama
spirometry hutathmini kiasi cha hewa mtu awezacho kukitoa baada ya kuvuta hewa
kwa nguvu na kwa haraka kiasi gani.
Viwango huwa chini ya kawaida iwapo njia za hewa zina maumivu na zimesinyaa. Kipimo hicho cha spirometry pia hutumika kutathmini jinsi mgonjwa wa pumu anavyoendelea kupata nafuu au tatizo kuongezeka.
Hata hivyo kipimo hicho ni kwa ajili ya watoto wenye zaidi ya miaka mitano na watu wazima tu.
Baadhi ya vipimo vingine vinavyoweza kufanywa iwapo kipimo cha spirometry hakitaonesha tatizo ni:
Kipimo cha Kizio (Allergy test)
Husadia kugundua iwapo kuna vizio mbalimbali vinavyoathiri mwili wako.
Kipimo cha Mazoezi
Kugundua iwapo kuna mabadiliko yoyote katika njia ya hewa kutokana na mazoezi.
Kipimo cha Ugonjwa wa Kucheua na Kiungulia
Kipimo hiki ni muhimu pia kutokana na uhusiano uliopo kati ya kiungulia, kucheua na ugonjwa wa pumu.
Kipimo cha Picha ya Mapafu (X-ray)
Kipimo hiki pia hutumika kuona iwapo kuna kitu chochote kilichoziba njia ya hewa aukama kuna maradhi yoyote katika mapafu
au moyo.
Kutokana na vipimo daktari wako atapata picha ya ukali wa pumu yako na kukuanzishia tiba muafaka.
Matibabu yapo na mtu mwenye tatizo hili anapona kabisa na hatosumbuliwa na tatizohilo
tena.
Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa sugu ambao huathiri njia za hewa ambazo huingiza na kutoa hewa katika mapafu. Upatapo ugonjwa wa pumu, kuta za ndani za njia ya hewa hupata maumivu (inflammation) na kuvimba.
Maumivu katika njia za hewa huzifanya kujihami kwa kusinyaa na hivyo kupunguza kiasi cha hewa kinachopita kwenda kwenye mapafu. Hali hii husababisha muathirika kutoa mlio
Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa sugu lakini unaotibika. Unaweza kudhibitiwa
Aina za Pumu
Kuna aina kuu mbili za pumu. Aina ya kwanza ni ile inayoanza mapema (early onset asthma) na aina ya pili ni ile inayochelewa kuanza (late onset asthma).
Kwa kifupi tutaenda kuangalia tofauti chache kati ya aina hizi za pumu.
Pumu inayoanza mapema
Ni kawaida kwa aina hii ya pumu kuanza utotoni na kwa kawaida huwatokea waathirika ambao miili
Waathirika wa aina hii ya pumu hutambuliwa kwa vipimo maalum vya ngozi ambapo huonesha kuathirika kwa asilimia kubwa vipimo hivyo vinapofanywa.
Pia waathirika hawa huwa na matatizo mengine ya mzio (allergic disorders)
Pumu inayochelewa kuanza
Aina hii ya pumu tofauti na iliyopita huanza katika umri wowote na asilimia kubwa ya waathirika ni watu wazima. Hakuna ushahidi wowote unaohusianisha vizio (allergens) vinavyotokana na mazingira na uwezo wa kusababisha aina hii ya pumu.
Pumu husababishwa na nini?
Bila shaka mpenzi msomaji umekua ukijiuliza swali hili mara kwa mara. Haifahamiki haswa ni sababu zipi zinazopelekea njia za hewa kupata maumivu na hivyo kupelekea mtu kupata pumu.
Vyanzo mbali mbali vinaonyesha kuwa inatokana na mseto wa vitu
Pia kuna vitu katika mazingira ambavyo vinaweza kusababisha mtu kushambuliwa na pumu. Vitu kama vile mazoezi, vizio, viwasho (irritants) na maradhi yatokanayo na virusi.
Baadhi ya vizio ni kama vifuatavyo:
-Vumbi
-Mende
-Chavua (pollen) kutoka kwenye miti na majani
-Magamba ya wanyama, manyoya n.k
Viwasho kama:
-Moshi wa sigara
-Uchafuzi wa hewa
-Harufu kali (kutoka kwenye rangi au chakula)
-Msongo wa mawazo
Vingine ni kama:
-Dawa kama Aspirin
-Ugonjwa wa kucheua
-Viwasho au vizio vitokanavyo na kemikali
-Magonjwa ya njia ya hewa n.k
Ieleweke kwamba orodha iliyotajwa hapo juu siyo kamilifu kwa maana kwamba haijasheheni vitu vyote vinavyoweza kuleta dalili za pumu na pia muathirika anaweza kuathirika na kimoja wapo au zaidi.
Vigezo hatarishi
Baadhi ya vigezo hatarishi vinavyoweza kuongeza uwezekano wa kusababisha ugonjwa wa pumu ni pamoja na:
-Kuishi katika miji mikubwa, haswa katikati ya mji ambapo huongeza uwezekano wa kukutana na vizio
-Kuvuta hewa iliyo na moshi
-Kemikali zitokanazo na kilimo, dawa za kutengeneza nywele, rangi, vyuma, plastiki au vifaa vya elektroniki
-Kuwa na mzazi mmoja au wawili wenye pumu
-Kuathirika na maradhi ya mfumo wa hewa kama kikohozi na mafua wakati wa utoto.
-Unene wa kupita kiasi (obesity)
-Ugonjwa wa kucheua na kiungulia (Gastro esophageal reflux disease)
Dalili za Pumu
Baadhi ya dalili za kawaida za ugonjwa wa pumu ni kama zifuatazo:
-Kikohozi: Mara nyingi kikohozi cha pumu huwa kikali nyakati za usiku au alfajiri na hivyo kumfanya mwathirika kutolala vizuri
-Kutoa sauti ya mfano wa mtu anayepiga mluzi au filimbi wakati wa kupumua
-Kifua kubana: Mgonjwa husikia kama kitu kinakandamiza kifuani au wakati mwingine husikia kama mtu amemkalia kifuani.
-Kukosa hewa: Baadhi hujisikia
-Kupumua haraka haraka
Ikumbukwe kwamba si watu wote huwa na dalili zilizokwisha tajwa hapo juu na dalili zaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu.
Dalili pia zinatofautiana ukali. Wakati kwa mwingine dalili zinakuwa za wastani, wengine zinakuwa za kukera tu au mbaya kiasi cha kumzuia muathirika kufanya shughuli zake za kila siku.
Vile vile wapo wengine ambao dalili zinakuwa mbaya kiasi cha kuhatarisha maisha. Dalili pia zaweza kutofautiana kwa kipindi zinapotokea.
Wengine hupata dalili mara moja tu kwa mwezi, wengine kila wiki na wengine hupata dalili kila siku.
Hata hivyo iwapo muathirika atapata matibabu sahihi anaweza kuishi na dalili chache au bila dalili kabisa.
Uchunguzi
Kipimo cha muhimu katika uchunguzi iwapo mtu ameathirika na pumu ni kuangalia jinsi mapafu yanavyofanya kazi.
Kipimo hicho kijulikanacho kwa lugha ya kitaalamu
Viwango huwa chini ya kawaida iwapo njia za hewa zina maumivu na zimesinyaa. Kipimo hicho cha spirometry pia hutumika kutathmini jinsi mgonjwa wa pumu anavyoendelea kupata nafuu au tatizo kuongezeka.
Hata hivyo kipimo hicho ni kwa ajili ya watoto wenye zaidi ya miaka mitano na watu wazima tu.
Baadhi ya vipimo vingine vinavyoweza kufanywa iwapo kipimo cha spirometry hakitaonesha tatizo ni:
Kipimo cha Kizio (Allergy test)
Husadia kugundua iwapo kuna vizio mbalimbali vinavyoathiri mwili wako.
Kipimo cha Mazoezi
Kugundua iwapo kuna mabadiliko yoyote katika njia ya hewa kutokana na mazoezi.
Kipimo cha Ugonjwa wa Kucheua na Kiungulia
Kipimo hiki ni muhimu pia kutokana na uhusiano uliopo kati ya kiungulia, kucheua na ugonjwa wa pumu.
Kipimo cha Picha ya Mapafu (X-ray)
Kipimo hiki pia hutumika kuona iwapo kuna kitu chochote kilichoziba njia ya hewa au
Kutokana na vipimo daktari wako atapata picha ya ukali wa pumu yako na kukuanzishia tiba muafaka.
Matibabu yapo na mtu mwenye tatizo hili anapona kabisa na hatosumbuliwa na tatizo
No comments:
Post a Comment