LAZIMA utokwe machozi! Grace John mkazi wa Mzumbe, Mvomero mkoani Morogoro yupo kwenye wakati mgumu kutokana na maradhi ya ajabu yanayomsumbua mwanaye Honolina Christian Mkude (11).
Mtoto
Honolina akipata kinywaji.
Honolina anasumbuliwa na ugonjwa wa kuota
nyama sehemu za mwili wake zinazofanana na pembe za mnyama, ugonjwa ambao
unamtesa tangu kuzaliwa kwake.ILIKUWAJE?
Akisimulia kisa kizima, mama mzazi wa Honolina, Bi. Grace, anasema tangu amemzaa mwanaye huyo ni mitihani baada ya mitihani.
Wasamaria
wema wakimpatia misaada mama Honolina.
Mazungumzo hayo yalifanyika hivi karibuni
katika kituo cha mabasi ya mikoani, Msamvu, mjini hapa wakati mama huyo na
mwanaye wakihangaikia kuchangisha fedha za usafiri wa kwenda Moshi kutafuta
tiba zaidi katika Hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC).“Ndugu mwandishi, kwa kweli sijui hatima ya mwanangu. Nilimzaa akiwa ameota nywele sehemu zote za mwili wake, hadi usoni. Mimi na mume wangu tulishangaa, lakini tuliendelea na matibabu katika hospitali mbalimbali maana baadaye alianza kupatwa na uvimbe.
Honolina
Christian Mkude (11) anayesumbuliwa na ugonjwa wa kuota nyama.
MTIHANI MWINGINE“Jamani ndugu yangu... Mungu ana mitihani yake. Mume wangu (Christian Mkude) ambaye ndiye alikuwa tegemeo pekee kwetu, alifariki mwaka 2007 kwa ajali ya gari, wakati akisaka fedha za matibabu ya mwanetu.
“Kifo chake, kwangu kimekuwa pigo mujalabu. Sina pa kukimbilia na hivi juzi tu tulikuwa tumelazwa Hospitali ya Mkoa (Morogoro) na hapo tumepewa barua ya kwenda KCMC kwa matibabu zaidi.
Mama
Honolina akipokea msaada kutoka kwa msamaria.
“Hivi unavyoniona nachangisha fedha ili
nipate angalau nauli za kutufikisha kwanza hospitalini. Nimechanganyikiwa
kabisa,” alisema Bi. Grace kwa majonzi na kuongeza:“Wakati tatizo la mwanangu linaanza sikutegemea
Mtoto
Honolina (kulia) alipoanza kuugua.
SAUTI YA BI. GRACE KUTOKA MOSHIMisaada ya fedha kidogo alizopata kwa wasamaria wema waliomuona Msamvu, ulimsaidia mama huyo kusafiri hadi Moshi na kufika katika Hospitali ya KCMC.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Moshi, Bi. Grace alisema: “Nawashukuru waliniosaidia, tumefika salama na mwanangu hapa KCMC, ndiyo tumeanza taratibu za matibabu.”
BADO ANAHITAJI MSAADA
“Madaktari wametupa moyo, wamesema watajaribu kumsaidia mwanangu. Watamtoa hizo nyama ila kwa sababu kutabaki na mashimo lazima wapandikize nyama nyingine.
“Tumeshakubaliana kuwa mimi ndiye nitakayekatwa sehemu ya nyama kutoka kwenye makalio yangu kwa ajili ya kumsaidia mwanangu,” alisema Bi. Grace, kilio kikisikika kwenye simu.
Wananchi
wakimtazama Honolina kwa huruma.
Akaongeza: “Wameshachukua nyama za mwanangu
na kwenda kupima na baadaye watachukua zangu ili kuona “Watanzania wenzangu, naombeni mnisaidie ili niweze kuondokana na hili tatizo. Mimi ni mjane na sina kazi ya kueleweka, napigania uhai wa mwanangu. Naombeni msaada wenu,” alisema.
SHIRIKI BARAKA
Kumsaidia mhitaji wa kweli huongeza baraka katika kipato, vitabu vitakatifu vinaeleza wazi. Ndugu wasomaji wetu wapenzi, kwa yeyote atakayeguswa na mateso ya familia hii, anaweza kumsaidia chochote mama huyo kupitia simu zake namba 0719 749542 (Tigopesa) na 0762 425973 (M - pesa).








No comments:
Post a Comment