Mzee Nkwabi Ngobola Kapimbi (91) baada ya kufunga
pingu za maisha na mkewe Maria Mkiwa (78).
Jelard Lucas na Hamida HassanMwaka mpya mambo mapya.
Katika tukio linaloweza
kuitwa kama ndoa ya karne, mzee mmoja mwenye
umri wa miaka 91, Nkwabi Ngobola Kapimbi, wiki iliyopita alifunga pingu za
maisha na mkewe Maria Mkiwa (78) mbele ya mchungaji Thobias Shilole wa Kanisa
la Maombezi…
Jelard Lucas
na Hamida HassanMwaka mpya mambo mapya.
Tukio hilo lililovuta hisia za watu wengi, lilitokea baada ya wanandoa hao kutimiza miaka 55 tokea walipoanza kuishi pamoja, katika uhusiano ambao walibahatika kupata watoto saba, wajukuu 78 na vitukuu 24.
Akiwa amevalia suti huku mkewe akiwa ndani ya vitenge, mzee Nkwambi alisema amejisikia furaha sana kufanya kitendo hicho kwani ni jambo ambalo kwake na la tatu kwa umuhimu, mengine yakiwa ni kuzaliwa na kifo.
“Watu wengi wanauliza tulikuwa wapi siku zote hizi, ni kwamba nilikuwa simuamini
Alisema hajali kama kuna watu watakuwa wakizungumza wanalojua kuhusu ndoa
“Mara ya kwanza mke wangu alikuwa anasita, lakini nilisema lazima tukafunge ndoa kwenye kanisa la Mzee wa Upako ( Antony Lusekelo), nampongeza mchungaji Thobias Shilole kwa kuwa pamoja nasi na kukubali kubariki ndoa yetu, lilikuwa jambo la furaha kwangu na mke wangu,” alisema Babu Nkwabi.
Kwa upande wake, mkewe Maria alisema awali alikuwa akisita kwa kuona kama itakuwa ni kituko mbele ya jamii, lakini baada ya majadiliano na mumewe, akaridhia jambo
“Najua maneno lazima yasemwe lakini mimi nampenda


No comments:
Post a Comment