Unaikumbuka hiii ya mwaka 2013????
MKE wa
Rais mama salma Kikwete amezindua wodi la
kisasa la huduma ya wanawake na watoto
katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa
Iringa huku akipongeza jitihada kubwa
zilizofanyika katika Hospital hiyo katika kuboresha huduma ya
mama na mtoto.
Mbali ya
kuzindua jengo hilo bado mama Salma Kikwete
amewashukia wakazi wa mkoa wa Iringa ambao
wanaendelea kuongeza kasi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI
kwa kusaliti ndoa zao na kuwataka kuacha mara moja.
Akifungua
wodi hilo leo Mama Kikwete alisema kuwa serikali
imelenga kuendelea kuboresha huduma ya afya na kuwa
mbali ya kuboresha majengo bado serikali imeendelea kuboresha
elimu ya watoa huduma kama njia ya kuboresha zaidi
huduma ya afya.
Hata hivyo
alisema changamoto za madawa na madaktari serikali itaendelea
kushughulika na kuwataka wanawake kuendelea
kutumia majengo hayo na kuepuka kuwapeleka watoto kwa
waganga wa kienyeji ama wao kujifungulia majumbani .
Kwani
alisema kukamilika na kuboreshwa kwa huduma hizo
ni kuepusha wazazi na watoto kuendelea kuwa na
fikra potofu kuwa watoto wao wamelogwa pindi
wanapokosa huku wakiacha kufika hospital na badala
yake kwenda kwa waganga wa jadi.
Katika
hatua nyingine aliwataka viongozi na wananchi wa
mkoa wa Iringa kuendelea kuyatunza majengo hayo
ambayo yamejengwa kwa fedha za wahisani .
“ kumekuwa na tabia
ya baadhi ya wananchi kuhujumu miundo mbinu ya
serikali kwa kuiba vifaa mbali mbali kwa madai kuwa ni mali
ya serikali …..hili si jambo jema lazima
wote tushirikiane katika vifaa hivyo ambavyo ni mali ya
watanzania wote”
Mama Kikwete
amesema kuwa kwa upande wake ataendelea
kutoa ushirikiano kwa Hospital hiyo katika
kutatua changamoto mbali mbali ikiwemo ya ushauri na kufikisha
changamoto hizo sehemu husika.
Japo
alisema kuwa suala la uhaba wa madaktari serikali
ni suala ambalo tayari serikali imeanza
kulifanyia kazi ni pamoja na kuendelea kuongeza
madaktari katika kuwapa mafunzo madaktari wapya
ambao wataweza kuongezwa katika Hospital hapa nchini.
Alisema kuwa
maambukizi ya UKIMWI Iringa ni asilimia 9.1 ambapo
ni sawa na watu 9 kati ya 100 mkoani Iringa
wameathirika idadi ambayo ni kubwa kuliko ile ya taifa
ya wastani wa watu 5 ambao wameathirika hivyo
mkoa wa Iringa bado upo juu kwa maambukizi hayo.
“ Watu
wa Iringa ari zaidi nguvu zaidi mmeiwaka
katika maambukizi ya UKIMWI hivyo nawaombeni sana watu
wa Iringa kujilinda zaidi na kuepuka kusaliti
ndoa zenu na wale ambao bado kuona ama kuolewa
basi kujiheshimu zaidi”
Pia
aliwataka wananchi wa mkoa wa Iringa kujenga
utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara
na wale ambao watabainika wameathirika
wasisite kutumia dawa za kufubaza virusi
vya UKIMWI na kuachana na tabia ya kuacha matumizi
ya dawa hizo.
Huku wale
ambao bado hawajaambukizwa basi kutulia na
kujilinda ili wasipate maambukizi hayo na kuwaomba
wanawake wajawazito ambao watakubwa na maambukizi ya
VVU basi kufika Hospital na kupima ili kuwezesha watoto
kuzaliwa bila maambukizi.
Wakati
huo huo mama Kikwete aliwataka wanaume ambao bado
kupatiwa huduma ya Tohara kujitokeza kufanyiwa
huduma hiyo ili kusaidia kupunguza
maambukizi ya VVU.
No comments:
Post a Comment