BAADA YA KANGA MOKO NDEMBE NDEMBE SASA HIVI NI MWENDO WA T SHIRT NDEMBWE NDEMBWE...!!
KWA muda mrefu,
zilisikika sauti za kupiga vita makundi ya wanawake
yaliyosifika kwa kucheza utupu kwa kulowanisha khanga maji maarufu kama Khanga
Moko Ndembendembe lakini sasa imeibuka nyingine, inayoitwa Fulana au Tisheti Ndembendembe Uchunguzi wetu wa
miezi kadhaa tangu mwaka jana ulibaini kwamba tayari staili hiyo ya uchezaji wa
muziki wa mwambao kwa kulowanisha tisheti laini nyeupe kwa maji na kusababisha
chuchu kuonekana sawia, inazidi kushika kasi kama moto wa kifuu Bongo. Ilibainika kuwa staili hiyo ambayo ilianzia Pwani
ya Kenya,
sasa inatumiwa kudhalilisha warembo Uswahilini hasa kwenye ngoma maarufu za
‘kigodoro’ ambazo huchezwa bila kujali rika mbalimbali zinazokuwa zimechanganyikana.
Habari zilisema kuwa katika uchezaji huo, sharti ‘nido’ ya mrembo iwe saa sita
ili kuwavutia na kuwaridhisha wanaume kimahaba ambao kazi yao huwa ni kuwatuza fedha baada ya
kufurahishwa kwa kutazama uchezaji huo na wengine kuondoka nao kwenda kuvunja
amri ya sita. Ilifahamika kuwa staili hiyo imewavutia wengi na
vikundi vya uchezaji huo vimeanza kuundwa japo havijapata umaarufu mkubwa. Mamlaka na wizara husika zinatakiwa kukemea kwa
nguvu zote kwani huo ni mwanzo mwingine wa mmomonyoko wa maadili ya Kitanzania
na ongezeko la maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU).
No comments:
Post a Comment