MTUNZI:
Fortunatha Sixberth
MWANDISHI: ngoogle
Shakur +255712 554 944
Email:
ngogoshakur@yahoo.com
SEHEMU YA KWANZA
01
K
|
elele za nguvu
zilisikika kutoka katika chumba Kadri
zilivyozidi kuendelea ndivyo umati wa watu ulivyozidi kufurika kuelekea eneo
lile. Ama kwa hakika ilikuwa ni kama sinema ya
aina yake kwa mchana ule.
‘Amezoea huyu,
leo wacha nimuoneshe kuwa mimi ni zaidi yake’ sauti ya mwanamke ilisikika toka
mule ndani. Sauti ile ilizidi kuhamasisha waliokuwa nje ya chumba kile kutaka
kujua kulikoni? Lakini muda ulizidi kuyoyoma na hakuna aliyepewa fursa ya
kuingia ili angalau aje kuwa shahidi wa kuusimulia umma uliokuwa pale juu ya
kilichokuwa kikijiri mule ndani. “Niachie basi mke wangu…” sauti nzito ya kiume
ililalamika toka ndani ya chumba kile ikishadidia mawazo ya waliokuwa nje kuwa
ndani ya chumba kile mlikuwa na mpambano mkali kati ya mwandamu wa kike na wa
kiume.
Wakati hayo
yakijiri, wadau baadhi toka kundi la waliokuwa nje walitoa wazo kuwa ni vema
kwenda kumtarifu mjumbe wa nyumba kumi ili aje kutoa amri ya kuvunja mlango ili
kumaliza mtafaruku ule kwa lazima bila ridhaa ya wahusika. Ndio ni kwa lazima
bila ridhaa ya wahusika kwakuwa wenyewe walifunga mlango na komeo zote na
hawakuwa tayari kuonesha wengine kilichokuwa kinajiri ndani mule.
Ghafla sauti ya
juu ilisikika‘maaaama weeee unaniuaaaaaa!
Hii ilikuwa ni
sauti ya mwanamke ikiashiria kuwa alichofanyiwa kilikuwa kinauzito sawa na
kumpotezea uhai wake.
Jamani tufanye
maamuzi magumu tuvunje mlango watakuja kuuwana hawa….sauti ya msamaria mwema
mmoja ilijaribu kuchangia wazo. Hapana wewe utakuja kutukanwa buuuure we unajua
ugomvi wa wapendanao? Huwezi jua unavunja mlango kumbe watu wamo katika raha
zao…..huyu allikuwa na wazo la tofauti kabisa. Mwingine naye aliibuka na lake
‘Msilete utani bhana, mi navunja mlango na kama
kitatokea chochote liwalo na liwe” alimalizia. Kweli bwana fanya hivyo….sauti
za akina mama pamoja na wadada zilisikika kuashiria kukubaliana na wazo la kaka
yule aliyeonekana kuwa na mwili wa kishababi ambao kama
angeamua basi ni wazi angeweza kufanya bila shaka kile ambacho amekitolea tamko
dakika chache zilizopita.
Akiwa anajiandaa
kufanya kile ghafla sauti zilitamka…Afadhali umefika, maana kila mtu alikuwa na
wazo lake hapa. Bila kujibizana na mtu mtu yule
alijisogeza kunako mlango na kugonga kwa nguvu….ngongongo! Kimyaa alirudia tena
na tena lakini waapi hakuna aliyejibu. Naomba Kijana mwenye nguvu avunje mlango
huu haraka…alisema mjumbe na bila
kupoteza wakati Kijana mmoja mwenye umbo lililojaza alijisogeza karibu na
mlango ule na aligeuka kutazama umma uliojaa pale kasha kimzaha aliruka kinyume
nyume na kwa kutumia makalio yake akauvamia mlango. Puuu! Sauti hiyo ilisikika
na bila chenga watu waliweza kuona japo kwa uchache mandhari ya ndani ya chumba
kile ambacho kilikuwa kikisikika sauti zenye kuashiria patashika nguo kuchanika
muda si mrefu uliopita. Naomba vijana watatu wenye nguvu ongozana nami pamoja
tukashuhudie kulikoni….mjumbe aliita kundi la vijana na hakukupita sekunde
tayari waliongozana kuingia ndani.
Mamaaa weee!
Huyu si mzima tena. Ameshakata pumzi huyu au sio bwana mjumbe? Kijana mmoja
alidadisi. “Bila shaka itakuwa hivyo lakini tusimalize kila kitu kwa uwa ssi
sio madaktari tuwaachie kazi hiyo wahusika watatupa jibu sahihi kabisa”
Mjumbe hakutaka
kupoteza muda ndani ya dakika tatu alipiga simu kituo cha polisi na difenda
ilikuwa tayari eneo la tukio kuchukua wahusika. Ndani ya diffenda kulikuwa na
afande Katosho ambaye alikuwa pamoja na
afanse wa kike Zipora. Kundi la mashuhuda lililokuwa hapo awali limezunguka
nyumba ile baada tu ya kufika gari la polisi lilionekana kusambaratika na
kuacha eneo lile kubaki na watu wachache huku umati ukiwa kwa mbali mbali.
Makamanda hawa
hawakutumia muda mwingi walishaingia ndani ya chumba cha tukio na punde vijana
waionekana wakibeba miili mitatu kuingiza katika gari. Miili ile ilionekana
wazi kuwa ni wanawake wawili na mwanamume mmoja. Gari la polisi liliondoka kwa
mwendo wa kasi ili kujaribbu kuokoa maisha ya wahanga wa tukio lile.
Umati uliobaki
eneo lile uliachwa na maswali mengi yasiyo na majibu…ni akina nani basi
waliokuwa katika tukio lile? Hali za watu wale zilikuwaje yaani ni wazima au
wote wamefariki? Na wengine walikwenda mbali zaidi na kujiuliza kisa namkasa
cha tukio lile. Lakini maswali haya hayakupata majibu kutokana na ukweli kuwa
wahusika ndio wale walikuwa hawajitambui wakati wakitolewa eneo lile na hata
wale vijana watatu waliosaidia pengine ndio angalau wangeeleza lolote nao
walichukuliwa na ili kwenda kusaidia taarifa muhimu kituoni.
Basi hakukuwa na
jinsi ilibidi kila mmoja achukue njia yake huku wabunifu wakijaribu kueleza
uongo usiosanifu juu ya tukio lile……………USIKOSE SEHEMU YA 2
No comments:
Post a Comment