Mswahili mwenzangu, ni kweli
kuwa kila mmoja ana mtazamo wake na upeo wake wa kufikiri lakini katika hili
wacha niseme kuwa Mtazamo huu siuungi mkono hasirani.
Kumekuwa na katabia kuwa
wapenzi (hasa wa kike) wanapofumaniwa KUTEMBEZWA UCHI HADHARANI ili
KUWAKOMESHA.
Ninachojiuliza ni kwamba
inakuwaje wewe unayemtembeza mwenzako hadharani kama
ingekuwa wewe ndiye uliyekutwa , UNGEKUWA TAYARI KUTEMBEA HADHARANI UCHI????
Mi nadhani kuna ADHABU nyingi
ambazo mwenza wako unapomfumania unaweza kumpa kama
moyo wako kweli umeshindwa kuvumilia tukio na aibu ile.
ADHABU nzuri kuliko zote ni
KUAMUA KUACHANA NAE KABISAA, sidhani kama
utaamua kuachana naye kuna aibu ambayo itaendelea kukuzonga mbali na yeye
mwenyewe ambaye ataendelea kuzongwa na aibu hiyo milele na milele.
Mswhili mwenzangu JAHAZI LA
MSWAHILI linawapa pole wale woote ambao wamepata kufikwa na ADHABU za namna
hiyo kwani ni kinyume pia na haki za kibinadamu, unayemtembeza hadharani ni
wazi kuwa hatakuwa na hamu ya kuendelea KUISHI ASILANI…..Kwanini adhabu yako
ipelekee kuondokewa na uhai kwa yule ambaye dakika chache zilizopita ulikuwa
Ukimthamini an kumpenda kwa kila hali?????
maoni yako ni muhimu msomaji wangu….
No comments:
Post a Comment