Mrembo huyu aliyejitambulisha
kwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu kimojawapo mjini Iringa
akilia baada ya kupokea kichapo kutoka kwa mwanamke mfanyabiashara
eneo la Miyomboni mjini Iringa baada ya kuiba viatu vya mtumba na
kuficha kwapani
Hapa akimpigia simu mpenzi
wake ili aweze kumkomboa baada ya kutakiwa kulipa Tsh 50,000 kwa
viatu pea mbili alizoiba .
Tukio la mrembo huyo kupokea
kichapo na kuvuliwa nguo na kupokonywa simu yake na mikoba
zaidi ya mitano pamoja na kiasi cha TSh 15,000 ambazo alikuwa
amezihifadhi limetokea jumapili wiki hii katika eneo la
Miyomboni mjini Iringa.
Akielezea
juu ya mkasa huo wa aina yake leo mfanyabiashara
huyo mama Masawe alisema kuwa eneo hilo amekuwa na kawaida
ya kuibiwa viatu katika duka lake la viatu vya
mtumba .....
Mama
huyu anadai kuwa mbali ya kukamatwa kwa
mrembo huyo bado amepata kukamata vijana zaidi
ya wawili watanashati ambao wamekuwa wakifika na kujifanya
wakichagua viatu na kuishia kuiba na kutoweka .
Binti
huyo ambaye ni mwanachuo alifika dukani
hapo na kuanza kuchagua viatu akijifanya ni
mteja .....
Baada
ya kuona muuza duka ameangalia pembeni,
binti huyo alichukua pea moja ya
viatu na kuificha kwapani asijue kwamba
pembeni kulikuwa na mtu mwingine aliyekuwa
akimwangalia....
Alipoaga
na kutaka kuondoka ndipo timbwili la kichapo lilipoanza
kwa mrembo huyo ambae aliomba asipelekwe polisi na
asipewe adhabu kubwa kwa kuwa ana ujauzito
wa miezi mitatu tumboni.
Alisema
kuwa kutokana na maombi ya mrembo huyo kupunguziwa adhabu
hakuweza kumfikisha polisi zaidi ya kumpa kichapo cha kufa
mtu na kumpokonya mali zote alizokuwa ametoka kuiba katika
maduka ya Miyomboni mjini hapa pamoja na simu yake ya kiganjani
.



No comments:
Post a Comment