Dec 5, 2013

MAVAZI YA NUSU UCHI WANAFUNZI WA KIKE KULIKONI????


MCHANO wangu unawahusu wadada ambao wako skuli lakini mavazi na mienendo yao haiendani na uhusika huo.

Utamkuta mwanafunzi katika sare za shule lakini alichokivaa ni BALAA TUPU. Mtoto wa kike amevaa sketi ambayo kama angechaguliwa eneo la kuwapo na kivazi hicho labda ni baa ambako angekuwa anafanya UBAAMEDI. Mtoto wa watu amekuvalia Kishati bila shaka kwa wazee wetu walioingia jijini wiki hii toka mkoani watakwambia ni Kishati cha mdogo wake lakini wapi ni cha kwake! Mwanafunzi huyo haishii hapo, anapaka kitu cha kumeremetesha mdogo wake kiasi kwamba UKIKUTANA NAYE hutakuwa na haja ya KUJIULIZA huyu si mwanafunzi kimaadili bali ni JITU ZIMA LINALOJIUZA kupitia KIVULI CHA UANAFUNZI.

SWALI LANGU; Nyakati zote niwaonapo wanafunzi wa namna hii hujiuliza Maswali haya
a)     Mwanafunzi wa namna hii asubuhi ya siku hii ametoka nyumbani kwa wazazi wake au atakuwa ametoka kwa bwana??? Kama ametoka kwa Mzazi basi ni haki kusema mzazi huyo hamtakii Mema mtoto wake NA kama atakuwa ametoka kwa bwana basi bwana huyo atambue kuwa kama alivyofanikiwa yeye kumnasa KINDA huyo na kumuweka ndani usiku kucha basi siku inayofuata atanaswa na mwenzake anayependa KINDA hilo tunaloambiwa ni taifa la kesho.
b)    Inakuwaje kwa walezi wa kule aendako (walimu). Ninastaaajabu kuona kuwa pamoja na kuvaa katika misingi ya namna ile lakini mwanafunzi huyu bado anaruhusiwa kuingia shuleni na kupatiwa elimu ambayo TUNADAI ndio MSINGI WA MAISHA YAKE.

ANGALIZO:
Kama tuna nia njema na kizazi chetu kijacho HATUNA BUDI kuchukua hatua za Makusudi dhidi ya tabia za nama hii. VINGINEVYO; tutawalalamikia Makondakta, walimu, maofisa na wadau wengine kuwa WANATUHARIBIA KIZAZI CHA KESHO. Cha msingi, kila mmoja katika nafasi yake ahakikishe ANACHUKUA HATUA kupambana na hali hii Mzazi, Mwalimu, Mwanajamii.

MSWAHILI NAFUNGA DOMO LANGU MIE LAKINI UKWELI NDIO HUOOOOO
Ukiwa na CHANO wako niandikie ngogoshakur@yahoo.com

No comments:

Post a Comment