Mama mzazi wa marehemu
‘Seven Kanumba’ Frola Mtegoa.
MAMA wa msanii nguli wa
filamu nchini marehemu ‘Steven Kanumba’ Frola Mtegoa amesema yuko katika
mkakati wa kuandaa filamu inayohusu maisha ya mwanaye kiasi cha kufikia hatua
ya kuomba msaada ‘kutembeza bakuli’. Akizungumza na paparazi wetu mama
huyo alisema kwamba, anapata wakati mgumu kukamilisha jambo hilo
kutokana na kukwama na kutaka asaidiwe ili kufanikisha jambo hilo .
“Nimekwama na nawaomba
wadau wajitokeze kunisaidia nikamilishe hili, nahitaji msaada wa kifedha na
hata ushauri,”alisema.
Mama huyo alisema lengo la
kuandaa kazi hiyo ni kutaka kufikisha ujumbe katika jamii kwa kuamini kwamba wengi watajifunza kupitia
maisha ya mwanawe.
Marehemu Steven Kanumba.
|


No comments:
Post a Comment