Dec 14, 2013

DENTI AKUTWA AKIJIUZA BUGURUNI…AFUNGUKA SABABU YA KUFANYA HIVYO


 
DENTI mmoja aliyefahamika kwa jina la Rehema mwenye umri
wa miaka 15, hivi karibuni alinaswa gesti akidaiwa kufanya
biashara haramu ya ukahaba.
Rehema alikamatwa katika gesti moja iliyopo maeneo ya
Buguruni Malapa jijini Dar kufuatia operesheni iliyoendeshwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum na baadae kufikishwaMahakama ya Hakimu Mkazi, Sokoine Drive kwa ajili ya
kusomewa mashitaka.
Baada ya kufikishwa mahakamani hapo, Mwendesha Mashitaka
wa mahakama hiyo, Richard Magodi alisema binti huyo hawezi
kufunguliwa mashitaka kwenye mahakama hiyo isipokuwa
anatakiwa kupelekwa kwenye mahakama ya watoto iliyopo
Kisutu jijini.
Hata hivyo, baadae binti huyo aliyekuwa amevaa kichangu
aliachiwa huru na alipozungumza na mwandishi wetu alidai
kuwa, akiwa kwa wazazi wake huko Mwanga mkoani
Kilimanjaro alichukuliwa na mwanamke mmoja aliyemtaja kwa
jina la Vero kwa lengo la kuja kumtafutia kazi.
“Baada ya kufika Dar, sikutafutiwa hiyo kazi
matokeo yake niliwekwa kwenye gesti iliyopo
Buguruni Malapa na kufanyishwa ukahaba,
” alisema
binti huyo.
Akaongeza kuwa, kutokana na mazingira magumu anayoishi
akipatikana mtu wa kumsafirisha hadi kwao, atashukuru.

No comments:

Post a Comment